Maneno hayo yamesemwa na Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa lindi bi. Cesilia Sostenes katika kikao cha mnada 6 wa zao la mbaazi kilichofanyika 21/09/2023 katika ofisi za chama hicho cha ushirika (RUNALI) kinachohudumia wilaya za Ruangwa,Nachingwea na Liwale.


Bi Cesilia alisema kuwa hadikufikia mnada wa 5 wa mbaazi jumla ya tani elfu 17 zilikusanywa huku wilaya ya nachingwea pekee ikikusanya tani elf 9 hivyo kuifanya wilaya hiyo kuwa ndio mzalishaji mkubwa wa zao hilo kimkoa na kuwaomba wakulima wa wilaya hiyo na wilaya zingine zinazohudumiwa na chama hicho kuongeza juhudi za uzalishaji kwani bado mahitaji ni makubwa kuliko uzalishaji.

Katika mnada huo jumla ya mbaazi zilizokusanywa zilikua kilo milioni 1,082,119 huku mahitaji yakiwa kilo miloni 4,192,119. Jumla ya kampuni 14 zilijitokeza kuomba kununua zao hilo ambapo bei ya juu ya mnada huo ilikua 1960 na bai ya chini ya ununuzi ikiwa 1950. Wakulima walikubalianana na bei hiyo hivyo kuruhuru mchakato wa manunuzi kuendelea.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: