Maafisa elimu kutoka mikoa nane ya Tanzania bara wametakiwa kuhakikisha kuwa wanawajibu wa kusimamia usalama wa watoto wawapo shuleni pamoja nakuhamasisha jamii kuwalinda watoto.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Charles Msonde wakati akifungua mafunzo ya kutoa muongozo wa programu ya mradi SEQUIP kwa maafisa elimu ambapo alisema kuwa jukukumu walilopewa ni jukumu kubwa kwa nchi ambalo ni kuwasimamia watoto, kuwalea pamoja na kuwapa walimu muongozowa kulea.
Dkt Msonde alieleza kuwa kazi ya kusimamia maboresho ya elimu ambayo wameianza mwaka huu sio kazi rahisi bali ni kazi ngumu kwani wamefanya kazi kubwa sana ya kusimamia majukumu yao katika mikoa na halmashauri zao ambapo wamewaongoza vizuri walimu kusimamia vema ufundishaji wenye tija katika shule.
“Matunda tunaanza kuyaona ya kazi zenu mnazozifanya , mmepewa jukumu la kuwasimamia malezi yawatoto wa nchi yetu walio katika shule zetu na kuwaongoza walimu wetu kulea na jukumu hili halijaanza leo bali tangu enzi za waasisi wa nchi hii, ”Alisema Dkt Msonde.
“ Walimu wanahakikisha watoto wetu wanakuwa na maadili mema , wana nidhamu, uzalendo wa kuweza kuishi katika taifa letu kwa misingi ya mila na desturi za nchi yetu na sisi kama walimu tumekuwa tukilifanya vizuri sana,” Alieleza.
Alifafanua kuwa kwa kuhakikisha kwamba mustakabali wa maendeleo ya taifa letu unenda vizuri, na hasa kuhakikisha serikali inaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia serikali ya awamu ya sita imefanya mambo ya kuhakikisha kwamba inafanya kila inaloliweza ili kuwepo na mazingira salama, yanayopendezesha na kuwezesha jukumu la ufundishaji ma ujifunzaji vizuri.
Aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha awamu ya sita maboresho ya elimu ya sekondari yamekuwa ni makubwa na yanaenda kwa kasi ambapo kwa kipindi cha miaka mitano, tangu mwaka juzi serikali imepanga na kuendelea kutumia zaidi Trilioni 1.2 kufanya maboresho mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweka mkakati wa shule mpya, nzuri, safi na salama 1026.
“Leo tunavyoongea hivi katika hizi shule 1026 ambazo zimepangwa kujengwa kwa kipindi cha miaka mitano mpaka shule zaidi ya 440 zimeshajengwa ambapo lakini serikali imeweka mkakati pia wa kujenga shule 26 za mikoa za wasichana za bweni na mwaka jana shule 10 zimeshapewa bilioni tatu tatu na simeshapata wanafunzi na mwaka huu zimeongezewa bilioni moja moja ili kukamilisha na ziweze kuchukua zaidi ya wanafunzi 1000,” Alieleza.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa SEQUIP Beatrice Mbigili alisema kuwa inawalazimu kutoa mafunzo hayo kwaanzia kwa maafisa elimu mikoa ili kuweza kutekeleza programu ya shule salama katika shule za sekondari Tanzania ambapo maafisa elimu sekondari ndio wasimamizi wakuu wa elimu hivyo ni vema wakaelewa kwa undani na kwa kina programu ya usalama.
Hata hivyo mafunzo hayo yametolewa kwa maafisa elimu mikoa na maafisa elimu sekondari kutoka mikoa nane ambayo ni Arusha, Tanga , Kilimanjaro, Dodoma, Iringa, Pwani,Dar es salaam na Manyara.
Post A Comment: