Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru) wilayani humo kufanya uchunguzi kuhusu mradi wa maji wa Sh1 bilioni uliokuwa ukitekelezwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) katika vitongoji 7 vya Kata ya Vumari.
DC Kasilda ametoa maagizo hayo wakati alipokwenda kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa wilayani humo, ikiwemo Miradi ya Maji, ujenzi wa Madarasa ya shule ya Msingi Mbono unaotekelezwa na Mradi wa boost utakaogharimu 181milioni.
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samiha Suluhu Hassani amejitahidi kutoa Fedha nyingi Sana kwa ajiri ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ikiwemo hii ya Maji ambayo ametoa sh 1bilioni kwa ajiri ya ukamilishwaji katika vitongoji hivi 7 lakini kwenye usimamizi wa Miradi hii kuna changamoto, na Wananchi wanashindwa kunufaika na Miradi, amesema Mkuu wa wilaya
"Takukuru naomba Mfuatilie haraka iwezekanavyo kuchunguza hili tujue ni kitu gani kinachofanya wananchi hawa wa vitongoji vitano kati ya saba wasinufahike na miradi ya Maji na ni kwanini Maji hayawafikii wananchi hao
Pamoja na Hayo yote Mkuu wa wilaya Kaslida Mgeni ametoa shukran za dhati kwa Mhe Rais Dkt Samiha Suluhu Hassani kuendelea kutupatia Fedha nyingi Sana kwa ajiri ya kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo na kuhakikisha Fedha zinazo tolewa na Serikali zitatumika vyema kwa kutekeleza Miradi inayokusudiwa
Pia manager wa Maji wilaya ya Same Abdallah Gendaheka amesema kukosekana kwa Maji katika vitongoji vitano ni kutokana na bahadhi ya wananchi kuharibu Miundombinu ya Maji na vifaa vya Maji lakini Mradi huo mkandarasi alimaliza muda mrefu sana hivyo amewahasa wananchi kutunza vyanzo vya Maji
Bahadhi ya wananchi wa kata ya vumali Wilayani humo Asha Abdallah na Herman Mgonja wamesema changamoto kubwa wanayopata ni Maji hasa kwenye hiki kipindi cha kiangazi ambacho wanaradhimika kunywa Maji yasiyo Safi na Salama
Post A Comment: