Na John Walter-Babati

Mbunge wa Babati vijijini Daniel Sillo amewataka Wazazi na walezi Kuwalinda watoto wao waliohitimu elimu ya msingi pindi wanaposubiri matokeo ya kuendelea na elimu ya Sekondari na vyuo vya ufundi stadi.

Ametoa wito huo akizungumza na Wanafunzi,walimu na Wazazi katika Mahafali ya 63 katika Shule kongwe ya Msingi Riroda wilayani Babati mkoani Manyara.

Wanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Riroda  waliosajiliwa ni 176 wavulana 76 na wasichana 100 lakini waliofanikiwa kuhitimu ni ni 151 pekee wasichana 93 wakiwa na wavulana 58 huku wengine wakikwama kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro sugu.

Katika Risala yao wahitimu walieleza kuwa wana ukosefu wa computer shuleni hapo ambapo Mbunge ameahidi kutatua kwa haraka changamoto hiyo na kutafuata namna ya kuboresha miundombinu ya madarasa ambayo mengi yamechakaa kutokana na ukongwe wake.

Amewashukuru wazazi kwa kuweka misingi mizuri ya elimu kwa watoto wao huku akiwataka kutimiza wajibu wao katika malezi ya pande zote ili kuwaepusha watoto kuingia kwenye vitendo visivyofaa vikiwemo vya mapenzi ya jinsia moja.

Afisa elimu kata ya Riroda Jenister Mfangavo afisa elimu kata ya Riroda amewataka Wazazi wawafundishe watoto wao stadi za maisha ili waweze kujitegemea  na kuishi vyema katika jamii.

Shule ya Msingi Riroda ni miongoni mwa shule  zilizoanzishwa enzi za Utawala wa mkoloni chini ya Chifu wa Waghorowa, ina jumla ya wanafunzi 1499, wasichana 681 na wavulana 720.


Share To:

Post A Comment: