Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd kwa kufungua ofisi mkoani Geita na kuona umuhimu wa kushirikiana na sekta ya madini hasa wachimbaji katika kuwapatia vifaa.


Kampuni hiyo imezindua ofisi iliyopo katika Soko Kuu la Dhahabu Geita na kukabidhi maroli matatu yaliyonunuliwa na wachimbaji katika wakati hu wa maonyesho ya Madini yanayoendelea mkoani humo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mavunde amesema itarahisisha shughuli za uchimbaji ili Watanzania washiriki kikamilifu katika sekta ya madini.

“Nawapongeza kwa kuamua kusogeza huduma karibu kabisa na wachimbaji, niwaombe muendelee kutanua wigo, wachimbaji ni waaminifu wanao uwezo mkubwa wa kuchukua mitambo kwa njia ya mkopo na kuirejesha,” amesema Mavunde.

Amesema pia mwaka huu Mkoa wa Geita umewekewa lengo la kukusanya maduhuli ya Serikali Sh bilioni 243 na ndiyo mkoa unaoongoza kwa mchango mkubwa wa maduhuli.

Mkurugenzi wa Masoko na Biashara wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Salman Karmali, amesema GF imepanga kuwafikia watanzania woote katika kanda tofauti na kwa kuanzi awameamua kufungua ofisi katika kanda ya ziwa itakayorahisihia wafanyabiashara na wadau a madiki kupata huduma zetu kwa uharaka

Pia Salman alisema hii yote ni matunda mazuri ya serikali ya awamu ya 6 kwa kuweza kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na kampuni hii kwa mwaka huu inalengo la kufanya uzalishari wa magari makubwa (trucks) kufikia magari 1,500 yanayounganishwa katika kiwanda chetu cha GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani na hizi gari tunazokabidhi kwa wateja hii leo ni ni ni gari zilizotengenezwa nchini Tanzania.

GF waliingia makubaliano na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambalo lina vifaa vya kuchoronga na kufanya tafiti huku kampuni hiyo ikitoa mashine na maroli.


Aidha amesema ku[itia mkataba huo GF itaweza kuwap[atia mitambo na maroli wachibaji wadogo na wakubwa ilik kuwakomboa chini ya usimamizi wa STAMICO
Mkurugenzi wa STAMICO amesema miongoni mwa mambo waliyokubaliana ni kusogeza huduma sehemu za wachimbaji na kuwauzia au kuwakodishia vifaa.


“Tukio hili ni utekelezaji wa mambo ambayo tulikubaliana, jambo lingine tulilokubaliana ni kukodisha vifaa pamoja na kuuza.
“Sekta ya madini inahitaji mtaji mkubwa au uwekezaji mkubwa, lakini inahitaji muda mrefu.

Ukimuangalia mchimbaji mdogo si lazima awe na resource (rasilimali) nyingi, anaweza akachimba bila kuwa na uwekezaji wa muda mrefu.

“Kwahiyo tukaona tukae pamoja tujadiliane tuone namna ya kumrahisishia mchimbaji mdogo asipate presha ya kuwa na mtaji mkubwa wa kumiliki trucks, bludoza ndio aweze kuchimba,” amesema.

Meneja wa Benki ya CRDB Geita, Efrosina Mwanja, amesema wanashirikiana na kampuni hiyo kuwakopesha wachimbaji magari na vifaa.Kwa mujibu wa Meneja huyo kupitia makubaliano hayo mchimbaji anayehitaji gari au vifaa kazi hutakiwa kuchangia asilimia 30 ya gharama kisha asilimia 70 hukopeshwa na benki hiyo.

“Tunawakopesha Watanzania, mfanyabiashara au mchimbaji, atachangia asilimia 30 ya gharama yote ya manunuzi ya gari au vifaa. Kwahiyo tunatoa asilimia 70 ya gharama zote na dhamana ni kile chombo ulichonunua,” amesema Mwanja.
Amesema pia wamekuwa wakiwapeleka wachimbaji wadogo nje kama vile China, Dubai na Uturuki kwa lengo la kujifunza na kupata ufanisi katika shughuli za madini.

Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilitoa tuzo kwa wadau mbalimbali akiwemo Waziri Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Geita kutambua mchango wao katika kuendeleza shughuli za kampuni hiyo.

Share To:

Post A Comment: