Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda akiambatana na Makamu Mwenyekiti Zainab Shomari wakimuombea kura Mgombea wa CCM Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Bahati Ndingo katika mkutano wa hadhara Kata ya Ubaruku.
Akizungumza leo katika mkutano wa hadhara ,Mwenyekiti Chatanda amewaomba wananchi wa Kata ya Ubaruku na wanambarali kwa ujumla kumpigia kura nyingi na za kishindo kwa Mgombea wa CCM ambaye atahakikisha analeta Maendeleo makubwa zaidi ndani ya Jimbo hilo .
"Mimi pamoja na wenzangu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT tumekaa siku sita katika Wilaya hii ya Mbarali tumeonana na akina mama na wananchi kwa ujumla wa Wilaya ya Mbarali tumeona jinsi wananchi wa Mbarali wanavyokipenda chama chao hivyo hatuna wasiwasi na Wana Mbarali katika kuichagua Chama Cha Mapinduzi",amesema.
Post A Comment: