Na. WAF - Mtwara
Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imejenga majengo ya huduma za dharura 128 na majengo ya Huduma za wagonjwa mahututi 78 kwa mwaka 2023 nchi nzima.
Dkt. Mollel ameeleza hayo leo Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akisalimia wananchi wa wilaya hiyo.
“Mwaka huu Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga majengo ya huduma za dharura 128 nchi nzima na majengo ya huduma za wagonjwa maututi 78 ili kusaidia wananchi kupata huduma hizo kwa urahisi”. Amesema Dkt. Mollel
Aidha, Dkt. Mollel amesema kuwa ujenzi wa majengo ya huduma za dharura na huduma za wagonjwa maututi kwa mwaka huu ambapo sekta ya afya yote imepewa trilion 6.7
Dkt. Mollel ameongeza kuwa kwa Mwaka huu X-RAY za kisasa 199 zimenunuliwa na kusambaza katika Hospitali kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi ambapo X-Ray moja ya kisasa inagharimu kiasi cha shilingi Milion 500.
"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepunguza Rufaa za kwenda nje ya nchi kwa kuwezesha Sekta ya Afya kutoa huduma za Sikoseli katika Hospital ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma na Hospitali ya Mifupa (MOI) iliyopo Jijini Dar es Salaam kwa kuwa na mashine yenye uwezo wa kufanya upasuaji wa unaondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa kupitia puani", ameeleza Dkt Mollel
Pia, Dkt. Mollel amesema kuwa mashine hiyo ya kufanya upasuaji wa unaondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa kupitia puani imegharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 21 hiyo ni ishara ya upendo wa Rais Dkt. Samia kwa watanzania katika kulinda Afya za Watanzania wasipate adha ya huduma za Afya.
Post A Comment: