Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wazazi Mkoani Shinyanga wamekumbushwa kushiriki kikamilifu katika malezi bora ya watoto wao ili kuwaimarisha katika hatua za ukuaji wa ubongo na kwamba hatua hiyo itawasaidia watoto kukua katika utimilifu wao.

Hayo yamebainishwa na mwezeshaji kupitia Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoa wa Shinyanga ambaye ni meneja miradi kutoka shirika la ICS Bi. Sabrina Majikata  pamoja na mambo mengine amesema ni muhimu wazazi, Baba na Mama kushiriki katika malezi bora ya mtoto.

Amesema ipo changamoto ya baadhi ya wazazi wa kiume (Baba) kushindwa kushiriki katika hatua mbalimbali za malezi bora ya mtoto kushindwa kufikia utimilifu wao katika maisha ya kila siku.

“Kuna changamoto kubwa sana katika suala la malezi hususan kwa ushiriki wa Baba inaonekana Baba ushiriki wake bado siyo ule ambao unaoridhisha katika malezi ya mtoto, unapozungumzia malezi wazazi wengi wanafikiri ni jukumu la mama peke yake lakini tunasema mtoto anapolelewa, kusikia sauti za wazazi wote wawili na kujifunza kupitia wazazi wote wawili inasaidia pia kuchochea ukuaji wa ubongo wake”

“Lakini wanaonekana ni watoto ambao inaonekana kwamba mwisho wa siku wanafikia mafanikio yao kwa urahisi zaidi ukilinganisha na wale ambao wanapata malezi ya mzazi mmoja peke yake kwahiyo wito kwa wababa ni jambo la msingi sana kushiriki kwa pamoja katika malezi ya mtoto”.amesema Majikata

Kwa upande wake mratibu na mwezeshaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imependekeza kujumuisha masuala ya watoto wenye ulemavu katika programu zote za makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya mtoto, kupitia na kuboresha sherea, sela na miongozo juu ya haki za mtoto mwenye ulemavu, kujengea uwezo kwa watoa huduma juu ya umuhimu wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto pamoja na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utambuzi na afua za mapema kwa watoto wenye ulemavu.

Bwana Tedson Ngwale pia ni afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga amesema ni muhimu jamii kutambua kuwa baadhi ya aina za ulemavu zinatatuliwa na utumiaji wa lishe bora ambapo ameeleza kuwa elimu itaendelea kutolewa ili jamii iweze kukabiliana na ulemavu.

Amesema kupitia programu hiyo elimu itatolewa kwa wazazi, walezi na watoa huduma namna ya kuwatambua watoto wenye ulemavu na waliohatarini kupata ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwezesha mtoto kupata huduma za marekebisho mapema.

Aidha Ngwale amesema elimu hiyo itaendelea kutolewa kwenye jamii katika suala la kuepuka mila na imani potofu zinazochangia ukiukwaji wa haki za mtoto mwenye ulemavu.

Kupitia Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoa wa Shinyanga mafunzo maalum yameendelea kutolewa kwa watoa huduma wa serikali wakiwemo maafisa ustawi wa jamii, maafisa maendeleo ya jamii, maafisa lishe, maafisa afya pamoja na maafisa elimu.

Vile vile mafunzo hayo yanatolewa kwa watoa huduma wa vituo vya malezi ya mchana ya watoto (wamiliki wa vituo pamoja na waalimu wao) lakini pia mafunzo hayo yanatolewa kwa kwa shule binafsi ambavyo vinavituo vya kuwalelea watoto wenye umri mdogo kabla hawajaaza darasa la kwanza.

Washiriki wameshukuru kwa mafunzo hayo huku wakiahidi kuwa mabalozi wazuri katika kufanikisha na kufikia malengo ya utekelezaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoa wa Shinyanga.

Mratibu na mwezeshaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Septemba 21,2023.

Mratibu na mwezeshaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Septemba 21,2023.

Mratibu na mwezeshaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Septemba 21,2023.

Mafunzo yakiendelea kupitia  Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Septemba 21,2023 katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.







Share To:

Misalaba

Post A Comment: