Na John Walter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo, amehitimisha Ligi ya mpira wa miguu Sillo Cup 2023 katika kata ya Kiru six.
Inakuwa ni kata ya nane kati ya 25 za Jimbo hilo kukamilisha ligi ambapo Kiru six imeibuka Mshindi kwa kuifunga Kimara 2-0, mchezo uliopigwa uwanja wa shule ya Msingi Kiru six.
Sillo amesema ni furaha yake kuona vijana wanakuwa bize na michezo kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Amesema kuwa kupitia michezo ataendeleza mshikamano na mahusiano kati ya Vijana, chama cha mapinduzi na Serikali.
Sillo amekabidhi jezi,mipira na fedha taslimu kwa timu ya kwanza hadi ya nne.
Vijana walioshiriki Michezo hiyo wamempongeza Mbunge kwa kuwakumbuka kwani ni muda mrefu wamekosa uhondo wa Michezo katika maeneo yao.
Post A Comment: