Ugonjwa kipindupindu umerejea tena ulimwenguni wataalamu wanasema ni miongoni mwa magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuua kwa masaa tu kama mgonjwa hajapata huduma inayostahili hasa kwa wale walioathirikia zaidi.

Licha ya athari kubwa za ugonjwa huo unaotapakaa kwa kasi, Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuna uhaba mkubwa wa chanjo ya ugonjwa huo duniani.

Nchi za Tanzania na Kenya, ni miongoni mwa nchi ambazo mamlaka zake za afya zilizotoa tahadhari ya ugonjwa huo lakini unaujua kwa kina ugonjwa huu unaoathiri mpaka watu milioni 4 kwa mwaka na kuua maelfu ya watu duniani.

Wilaya ya Arusha ina waakazi 617,631 kwa mujibu wa sensa yam waka 2022 wengi wa wananchi hawa Jiji la Arusha wanaishi katika Kata ya Muriet yenye wananchi zaidi ya elfu 60,209.

Wakazi wa Jiji la Arusha wanasumbuliwa na ugonjwa wa mlipuko Kipindupindu hali zinazowafanya wananchi hao kulazwa katika eneo maalum lililotengwa katika Hospital ya Rufaa ya Mount Meru.

Jasmine Joel ni mkazi wa ungalimited ambapo amesema ni kweli kuna kipindupindu ila hawa viongozi wetu hawataki kutangaza ila juzi tu ndio nimetoka kupona kwani kule tulikuwa tumelazwa zaidi ya wagonjwa arobaini wapo wanaopona na pia wapo wanaofariki na kila siku wanakuja wagonjwa wapya zaidi ya watatu.

“Viongozi wameamua kufanya jambo hili siri ndio maana tunaambiwa tusizungumze popote maana mji huu ni mji wa utalii tutaharibu swala nzima la utalii hivyo nimekaa hospital mpaka nimepona nimehudumiwa vizuri namshukuru mwenyezi mungu” alisema

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Levolosi amesema kumekuwepo na dalili za kuenea kwa ugonjwa huo kwa kasi katika maeneo ya kata yake lakini swala hili lipo kwa mkuu wa wilaya na ndiye mwenye taarifa zote kuhusiana na ugonjwa huo ila kwa sasa yeye hana majibu ya kuaminika.

“Hii kitu imekuwa siri sana na sijui kwanini wanaficha hata mimi nasikiasikia tu kwa watu na kwa madiwani wenzangu ila kwa kweli bado sijakutana na mwananchi wangu mwenye changamoto hiyo ila kwa sasa naomba unipe muda nilifuatilie nitakupa mrejesho ila taarifa sahihi nadhani atakuwazo mganga wa wilaya na mkuu wa wilaya maana hao ndio wanaofahamu maeneo yalipotengewa hawa wananchi wetu” alisema

Meya wa Jiji la Arusha Maximilan Iraghe amewataka watumishi wa Halmashauri kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuepuka uchafuzi wa vyanzo vya maji kwa kuoga, kufua pamoja na kutupa takataka ovyo kwani kuna kila sababu suala la usafi kupewa kipaumbele kwa uongozi wa jiji la Arusha na si kusubiri viongozi watoe maelekezo.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango katika ziara yake Jijini Arusha mwishoni mwa mwezi wa tano alielekeza uongozi wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha Jiji la Arusha linakuwa safi kwani ndio kitovu cha utalii, “Nimefika pale tengeru panapoanzia Barabara hizi mbili kuja mpaka mjini kumechafuka sana chupa na baadhi ya takataka zimetapakaa ana huko pembezoni mwa Barabara hebu jitahidini kuweka hili jiji liwe safi ni chafu sana”alisema

Ili kukabiliana na kipindupindu jamii inatakiwa kuepuka visababishi vyake ambavyo vingi vinatokana na tabia ya mtu kuwa mchafu,  ikiwemo kula kinyesi kibichi kwa kutonawa mikono anapotoka chooni,kula vyakula bila kunawa mikono na  kutotumia vyoo na kunywa maji yaliyochanganyikana na kinyesi.

 

Kuhusu Kipindupindu

Kipindupindu ni ugonjwa unaotokana na maambukizi katika utumbo mdogo wa binadamu uletwao na vimelea vya bakteria ambao hufahamika kitaalamu kama ‘Vibrio cholerae’.

Ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine na usipo tibiwa kwa haraka, mwathirika hupoteza maisha ndani ya saa chache.

Mtu huambukizwa kipindupindu kutokana na uchafu, hasa kunywa maji ama chakula kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya ugonjwa huo.

 

Dalili za ugonjwa

Dalili za ugonjwa wa kipindupindu ni kuharisha ghafla choo chenye majimaji (ambacho rangi yake ni kama maji ya mchele) na chenye harufu mbaya kama shombo ya samaki, kutapika pamoja na kupungukiwa maji mwilini.

 

Jinsi ya kuzuia kipindupindu

Miongoni mwa njia zinazofaa katika kuzuia milipuko ya ugonjwa huo ni kutumia maji safi na salama, hasa kwa kuhakikisha yanachemshwa na kuchujwa kabla ya kunywa.

Kunawa mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni na kabla ya kula, kufunika chakula kikiwa mezani, ili nzi wasitue juu yake pamoja na kujenga choo umbali wa angalau mita 30 kutoka chanzo cha maji.

Kutokana na msimu huu kuwa wa maembe, matunda ambayo huwa ni kichocheo kimojawapo cha vimelea vya ugonjwa huo, ni muhimu kusafisha matunda hayo na kuyamenya kabla ya kuyatumia.

Pia ni vema kwa wanaotumia maziwa yatokanayo na wanyama kuhakikisha wanayachemsha kabla ya kuyatumia na kuepuka kutumia nyama au samaki ambao hawajapikwa vizuri.

 



Share To:

Post A Comment: