Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiongea na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Halmashauri Wilayani hapo.
Akizungumza katika mkutano huo , Ndg. Mbunge amewakumbusha madiwani kuwa mbele katika kutatua kero za wananchi na sio kusubiri viongozi wanaowaita “wa juu” ili waje tatua kero katika maeneo yao. Mbunge aliwaasa wajumbe kushughulikia kero za wananchi katika maeneo yao pale zinapotokea bilq kupoteza muda.
Katika mkutano huo pia, Ndg. Mawazo Mkufya alichaguliwa kwa kura 19 kati ya 21 zilizopigwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo katika kipindi cha Mwaka mmoja na kamati za madiwani pia ziliundwa upya na kupata viongozi pia .
Post A Comment: