MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Comrade Mohamed Ali Kawaida amewataka vijana wa CCM Mkoa wa Arusha kuendeleza umoja na mshikamano walionao katika kukikuza Chama Cha Mapinduzi hicho.
Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti Kawaida amesema kuwa anawapongeza vijana wa chama hicho mkoa wa Arusha kwa kuendelea kufanya shughuli za Chama Kwa ushirikiano mkubwa na wenye malengo makubwa ya kuendelea kuimarisha jumuiya hiyo ya UVCCM.
Kawaida amewataka viongozi wa UVCCM kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kutatua changamoto za kiuchumi Kwa vijana wa mkoa wa Arusha.
Pia Kawaida amesisitiza umuhimu wa Viongozi kuwasaidia vijana kutatua katika kutatua matatizo yao ya kiuchumi
“Vijana wana imani kubwa na Nyie viongozi nendeni mkawasaidie kutatua matatizo yao ya kiuchumi “ Alisema Kawaida
Mwenyekiti Kawaida amemalizia kwa kuwapongeza viongozi wa UVCCM mkoa wa Arusha kwa kufanya ziara zenye tija za kuendelea kuimarisha uimara Jumuiya na chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Arusha.
Imetolewa na Idara ya Hamasa na Chipukizi Mkoa wa Arusha.
Post A Comment: