Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga kimepata katibu mpya Bi. Odilia Batimayo akichukua nafasi ya Bwana Donard Magesa ambaye amestaafu.

Akizungumza baada ya kuwasili kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Septemba 17,2023 katibu huyo Bi. Odilia Batimayo ameahidi kukitumikia chama hicho kwa uaminifu mkubwa huku akiomba ushirikiano kutoka kwa viongozi na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Mkoa huo kwa ujumla.

Batimayo amesisitiza viongozi na wanachama wa CCM kushirikiana kwa dhati hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

Akizungumza katika hafla fupi ya kumpokea katibu mpya wa CCM Mkoa wa Shinyanga, katibu wa siasa, itikadi na uenezi wa chama hicho Mkoa wa Shinyanga Bwana Richard Masele amemhakikishia ushirikiano katika kuunga mkono juhudi za serikali kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Katibu mpya wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo akisalimiana na viongozi baada ya kuwasili katika ofisi ya CCM Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Septemba 17,2023.

Katibu mpya wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika ofisi hiyo leo Jumapili Septemba 17,2023.

Viongozi wa CCM na jumuiya zake Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika hafla ya kumpokea katibu mpya wa CCM Mkoa huo leo Jumapili Septemba 17,2023.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: