Kamati ya Utekelezaji ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) imetembelea Maskani ya CCM ya Dkt Mohammed Ali Sheni Iilyopo Wadi ya Jojo Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katika Ujenzi wa Taifa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa imechangia kiasi cha Shilingi Laki tano kwa ajili ya kuunganisha umeme katika jengo hilo.
Sambamba na hilo wakati anazungumza na wanachama na wananchi wa Jojo Komredi kawaida amewapongeza kwa kujitokeza kwa wingi na kusisitiza uwepo wao ni ishara ya kuwa Uhai wa Chama katika Wilaya ya Wete upo imara.
Aidha Komredi Kawaida amewashukuru sana kwa kuwasihi wananchi kuendelea kuwaunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa wanazozifanya za kuwaletea maendeleo.
Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya ya Umoja wa Vijana, Kusikiliza hoja na Changamoto za Wananchi na kuzitatua, pamoja na kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya CCM Mikoa ya Pemba ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020 - 2025 pamoja na miradi ya Chama na Jumuiya zake.
Post A Comment: