Na Denis Chambi, Tanga.
KAMATI ya Bunge ya elimu ,utamaduni na michezo imelipongeza shirikisho la mpira wa miguu Tanzania 'TFF' kufwatia uwekezaji unaoendelea katika ujenzi wa mradi wa vituo viwili vikubwa vya michezo vilivyopo Mnyanjani Tanga na Kigamboni mkoani Dar es salaam huku ikiiomba serikali kuona haja ya kujenga vituo vingine Kama hivyo mikoani.
Miradi hiyo mikubwa inayotekelezwa hapa nchini ambapo kwa Tanga ulianza kutekeleza rasmi 2020 na kukabidhiwa februry 2023 ukiwa tayari kwa awamu ya kwanza umekamilika katika ujenzi wa viwanja viwili hosteli pamoja na jengo la utawala .
Mara baada ya kukamilika TFF imedhamiria kuwekeza katika soka la vijana wa kike na wa kiume wenye umri kati ya miaka 4-23 ambapo vijana wa kike watakaopatikana katika mikoa mbalimbali hapa nchini wataweka kambi Kigamboni Dar de Salam huku wakiume wakiwa Mnyanjani jijini Tanga wakinolewa tayari kwajili ya michauano mbalimbali ya kuliwakilisha Taifa.
Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo leo September 9, 2023 akiwa pamoja na wajumbe wake mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya elimu, utamaduni na michezo Husna Sekiboko ameipongeza serikali kwa mapinduzi makubwa inayoyafanya kupitia sekta ya michezo hususan katika mradi huo ambao unakwenda kukuza vipaji vya wachezaji ,makocha ambao ni hazina ya Taifa la baadaye.
Ameipongeza TFF kwa kuendelea kusimamia maendeleoya mpira wa miguu hapa nchini hasa katika kipindi hiki ambapo timu za Taifa zinaendelea kufanya vizuri kimataifa ikikubukwa kuwa ni siku chache tu zimepita tangu Taifa Stars ilivyofuzu kwenda kucheza michauano ya Afcon 2024 nchini Cameroon.
Sekiboko ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga alilisisitiza shirikisho la mpira miguu Tanzania 'TFF' kuendelea kuimarisha mahusiano baina yao na wizara ya michezo ili kuweza kusimamia na kufanikisha maono na mipango ya serikali katika kutaka kuleta maendeo kupitia sekta hiyo.
"Kwa niaba ya kamati hii nimpongeze sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa nguvu kubwa anayoitumia katika kuwezesha sekta ya michezo tumeshuhudia katika michauano ya vilabu mbalimbali lakini hata katika timu zetu za Taifa amewekeza fedha nyingi na ameonyesha nia ya dhati ya kutaka kuendelea michezo nchini ". amesema Sekiboko.
Niwapongeze Sana TFF kwa mipango mikubwa mnayoifanya hadi leo tunaona timu zetu za Taifa zinafanya vizuri niwaombe sana kudumisha mahusiano ni jambo la msingi sana , mnafanya kazi nzuri sana sio tu katika miradi ya ujenzi lakini hata katika kuzinoa timu zetu za Taifa tumeona sasa Tanzania inavyunja mwiko kwa kutoka nje ya mipaka na kufanya vizuri tunawapongeza sana endeleeni na jitihada hizo za kuhakikisha kwamba timu zetu za Taifa zinaendelea kufanya vizuri" aliongeza.
Akizungumza naibu waziri wa wizara ya Sanaa utamaduni na michezo Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' amesema kuwa wizara itaendelea kuhakikisha michezo yote hapa nchini inapewa kipaumbele na kupitia vituo hivyo itakuwa ni njia bora ya kuwapata wachezaji wenye vipaji watakaokuja kushindana katika medani za kimataifa.
"Tunaona umuhimu wa kufanya mambo makubwa namna hii kwa sababu tunaamini vituo hivi maendeo makubwa ya mpira wa miguu hapa nchini, moja ya mipango ambayo tunayo kwa sasa hivi Kama serikali ni kujenga kituo kikubwa cha michezo ambacho kitasaidia kufundishia walimu wanaokuja kufundishia michezo huku mashuleni na vyuoni na serikali tunahakikisha kwamba maendeo yanaendelea kufanyika" alisema Mwana FA.
Post A Comment: