Kadogoo amekutwa na hatia ya kumwita mwizi Sanare ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) mkoani Arusha
Umuzi huo ulioandikwa kwenye kurasa 18 umetolewa leo, Septemba 15,2023 na hakimu Mkazi, Asia Ndossy wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha aliyekuwa akisikiliza shauri hilo la madai namba 23/2022.
"Kwa kuwa hana uthibitisho kwamba yale yaliyosemwa kwenye ile video yalikuwa ya uongo au kutengenezwa tunaona maneno hayo yalikuwa ya uongo kwa lengo la kumuumiza mdai hivyo maneno haya yamemuumiza mdai," amesema Hakimu Ndossy akitoa uamuzi huo na kuongeza.
...Mdaiwa anakiri kuwa mdai alikuwa na nyadhifa mbalimbali kuwa alikuwa mwenyekiti CCM, Mkuu wa mkoa na mkurugenzi wa shule ya Nanina Memorial hivyo alikuwa ameshajenga 'status' yake japo kwa sasa ni mtu wa kawaida hivyo amepata madhara,".
"Ni mtu anaweza kutegemewa na jamii kwa ushauri na maelekezo lakini kwa kupitia hiyo video/clip hiyo ilisambaa na upande wa wadaiwa hawakuweza kuonyesha kuwa iliishia katikati hakuna mtu mwingine aliweza kuiona,".
"Mdai atalipwa kama alivyoomba fidia milioni 200 kwa kumtukanwa na kukashifiwa , atalipwa shilingi milioni 50 kwa kupoteza hadhi yake pianmdai atalipa gharama ya shauri hili,".
Mahakama iliangalia endapo maneno aliyosemwa na mdaiwa ni ya kashifa na kama ni kweli mdai amedhurika na ana haki ya kulipwa na ameweza kuthibitisha kama kweli mdai alitendewa kitendo hicho.
"Kiini cha madai haya ni video au clip ambayo mdai aliileta mbele ya mahakama na ikapokelewa kama kielelezo kiliwekewa mapingamizi lakini nilisema nitayajibia kwenye hukumu," ameeleza hakimu huyo na kuongeza.
...Tukiangalia uhalisia wa 'youtube' mtu yeyote anaweza kuingia 'youtube' na 'kudownload' na kuangalia. Youtube dunia ina 'access' mahakama ilitegemea kupata mapingamizi zaidi kutoka upande wa wakjibu maombi kuwa video haikuwa youtube au haijawahi kuwepo lakini hawakufanya hivyo,".
"Upande wa wadaiwa walitakiwa kuonyesha video hiyo si halisi kwa kuleta mmiliki wa onoine hiyo aseme haikuwa hiyo hawakufanya hivyo video hiyo ni sahihi,"
Hakimu Ndossy ameendelea kueleza kuwa amefanya rejea kwenye kamusi ya sheria kuangalia maana ya neno kashfa akaona ni maneno ya uongo ambayo yanaweza kumletea chuki kwenye jamii au kudharauliwa sehemu anayoishi biashara na shughuli zake.
Pia amerejea sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 inasema kuwa kashfa ni taarifa yoyote itakayochapishwa au kutangazwa kwa lengo la kumuumiza mtu mwenye akili timamu kwenye jamii ambapo maneno hayo yanatakiwa yawe ya uongo.
"Tunakutana na maneno 'ndugu yangu Sanare amejiongezea eka moja na pointi kwenye eneo ambalo hajapewa..huu ni wizi imekuwa mambo ya kujirudiarudia sana kwa kiongozi huyu'yakisemwa na mdaiwa kama mwenyekiti wa halmashauri lakini hakuna muongozo wowote ulioletwa kwenye mahakama hii kama hotuba iliyoandaliwa na kamati kuwa maneno hayo yaliandaliwa kwa ajili ya kusomwa na mwenyekiti huyo wa halmashauri," anaeleza hakimu Ndossy akisoma uamuzi huo.
Amesema kuwa hakuna mahali pameletwa uthibitisho kuwa mdai aliwahi kupata uthibitisho wa tuhuma hizo na kuwekwa hatiani hivyo inathibitisha kuwa ni ya uongo.
Amesema kuwa "ili kuthibitidha kashfa inapaswa maneno hayo yanatakiwa yaelekezwe kwa mtu mdai anasikika kwenye video hiyo akisema "huu ni wizi imekuwa mambo ya kujirudiarudia sana kwa kiongozi huyu" inaonyesha kuna mtu anaelekea na kuna sehemu anasema ndugu yangu Sanare inamaana ndiye aliyekuwa anakusudiwa na maneno hayo,".
"Maneno hayo yanatakiwa kusambaa kwenye jamii kwa nija ya magazet,i video, TV, mikutano ya hadhara .
Kusambaza maneno hayo ni njia ya kuhalalisha tuhuma hizo za kashfa kwa kuwa inafanya jambo hilo kuelewa na kushika maneno hayo na kuweka kwenye akili zao kuwa mtu huyu mwenye tabia inayojirudia,".
"Mdaiwa kuongea mbele ya online tv juu ya tabia za mdai inaonyesha kuwa alisambaza ikafika 'youtube' 'ikauploadiwa' ina maana jamii iliona jambo hili hivyo Madai hayo yalithibitishwa bila kuacha shaka,".
Akiongea mara baada ya uamuzi huu, Sanare aliishukuru mahakama kwa kutenda haki na kutaka hukumu hiyo iwe fundisho kwa viongozi wenye madaraka kuheshimu wananchi wote na waelewe madaraka waliyo nayo ni ya muda tu.
Sanare alieleza kuwa suala hilo limefikia hapo kutokana na Kadogoo kukataa suluhu kabla ya suala hilo kufika mahakamani kwani aliitwa mara tatu na Malaigwanan wakimtaka aombe msamaha yaishe akakataa.
Hata hivyo Kadogoo mara baada ya uamuzi huo aliondoka mahakamani hapo huku akiwa hayuko tayari kuzungumzia uamuzi huo
Post A Comment: