Hata hivyo Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa wameanzisha rasmi mahusiano na Jeshi la Polisi ambapo wanaenda kutoa kwa kushirikiana na chuo cha Polisi Moshi kutoa kozi nne katika maeneo ya teknolojia ya ulinzi sanjari na ulinzi wa mtandao.
Kwa mujibu wa Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa wataenda kutoa Shahada ya Usalama wa kimtandao na Shahada uzamili katika fani ya mkakati wa mafunzo ya ulinzi (strategy study) na Shahada ya pili ya Usalama (Peace Security).
Vile vile chuo hicho kimeendelea kuboresha kituo atamizi kwenye fani za Benki na kuzalisha makampuni ya wanafunzi mawili Mood Uji na kido ambapo kwa mwaka ujao wanatarajia kuongeza zaidi
Amesema kwamba wanatarajia kukamilisha ujenzi wa hosteli za wanafunzi sanjari na mikakati mipya kupitia mradi wa heat unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 21 ambapo fedha hizo zinaenda kuboresha chuo hicho cha uhasibu Arusha na kuboresha miundombinu katika campus ya Manyara na kujenga cumpus mpya Songea.
"Sasa hapa Arusha ni ujenzi wa kituo cha kimkakati cha ICT na Lengo letu sisi ni kuhakikisha kwamba kwa kuwa sisi ni chuo cha Uhasibu na mambo ya fedha na ujasiriamali lakini sisi pia tupo chini ya Wizara ya fedha na tunawajibika kutoa msaada wa kitaalamu kwa sekta nzima ya kifedha" Alisema
Kwa mujibu wa Prof Sedoyeka amesema mwaka ujao wa fedha wanaenda kuboresha na kukamilisha miradi ya Ujenzi katika cumpus za Babati Dodoma na kuanza Ujenzi cumpus ya Songea sanjari na kuongeza ubora wa mfumo wa elimu inayotelewa chuo ni hapo (ISO 21001).
Post A Comment: