Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeanza kutoa mafunzo kwa watumishi wake kuhusu mfumo mpya wa manunuzi wa Nest, ambao unalenga kuboresha na kufanya manunuzi ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kuwa rahisi, haraka na yenye uwazi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Denis Mtasiwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ugavi - MZRH amesema kuwa Uongozi wa hospitali umeratibu mafunzo kutolewa kwa watumishi wa hospitali katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wale wa Idara ya Manunuzi, Fedha na Mipango kwa lengo la kuhakikisha kuwa watumishi wanajua jinsi ya kutumia mfumo huo mpya kwa ufanisi.
Ameeleza kuwa mfumo wa manunuzi wa Nest unatumia teknolojia ya kisasa ya mtandao na unaruhusu watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kufanya manunuzi kwa njia ya mitandao, hii inamaanisha kuwa manunuzi yanaweza kufanyika kwa haraka na kwa uwazi zaidi.
Mtasiwa ameeleza kuwa Serikali imewekeza kwenye mfumo huu mpya wa manunuzi utasaidia kupunguza matumizi ya fedha za umma na kuhakikisha kuwa manunuzi yanafanyika kwa njia ya uwazi na kwa kuzingatia sheria na taratibu za manunuzi kwa hiyo, ni muhimu kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kufahamu jinsi ya kutumia mfumo huu mpya wa manunuzi ili kuhakikisha kuwa manunuzi yanafanyika kwa ufanisi na kwa uwazi zaidi.
Post A Comment: