Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota, akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru 2023 baada ya kukabidhiwa ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kuanza mbio zake wilani humo kwa ajili ya kutembelea, kuweka jiwe la msingi na kukagua miradi ya maendeleo Septemba 28, 2023.
................................................................
Thobias Mwanakatwe, MAMYONI
HALMASHAURI ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida
imefanikiwa kutoa mikopo ya Sh.milioni 108 ambayo ni sawa na asilimia 48 kwa
vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu hadi kufikia Juni mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni,Kemirembe Lwota, katika
risara yake jana ya utii kwa rais Dk.Samia Suluhu Hassan wakati kuhitimisha
mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo,alisema mikopo hiyo ni kati ya Sh.milioni
224.4 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo katika mwaka wa fedha
2022/2023.
Lwota alisema Mwenge wa Uhuru ukiwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni umetembelea na kukagua miradi yenye thamani ya
Sh.bilioni 1.236 ambayo ni ujenzi wa barabara ya Manyoni-Msigati yenye urefu wa
mita 700 kwa kiwango cha lami nyepesi kwa gharama ya Sh.milioni 589.
Mingine ni mradi wa uhifadhi wa chanzo cha maji Kaloleni ambao unahudumia
wakazi 5,271 waliopo katika mitaa ya Ujasiriamali,Mwanzi,Mitoo ya
Chini,Kaloleni na Samaria, kiwanda cha kisasa cha kubangua korosho kilichojengwa
katika kijiji cha Ilucha kilichojengwa kwa Sh.milioni 568,Zahanati ya kijiji
cha Mbwasa iliyojengwa kwa Sh. milioni 77.6 ambayo itahuhudumia wakazi 2,526.
Miradi mingine iliyotembelewa na Mwengenwa Uhuru
ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya elimu ya awali katik kinijicha Chikuyu yaliyojengwa kwa Sh.milioni 64.9
kikundi cha vijana cha Imani - Majiru ambao wamenunua pikipiki ya magurudumu
matatu na mradi wa madawati 300 yaliyonunuliwa kwa halmashuri ya Wilya ya
Manyoni kwa fedha za ndani Sh.milioni 21.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa
2023,Abdalla Shaibu Kaim, akizungumza baada ya kutembelea mradi wa maji
Kaloleni, aliwataka wananchi kulinda vyanzo vya maji kwa kutofanya shughuli za
kilimo na ufugaji ndani ya vyanzo hivyo.
Alisema ipo wazi kuwa hairuhusiwi kufanya
shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo vya maji mita 60 na kuwagiza viongozi wa
wilaya hiyo kuimarisha ulinzi ili visiharibiwe.
Post A Comment: