Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Raymond Mwangwala ameanza ziara ya Siku ya Kwanza Kata ya Pinyinyi ya kukagua miradi ya Maendeleo na Kusikiliza Kero za wananchi.

Mwangwala amepokea taarifa ya Maendeleo ya Kata ya Pinyinyi na kukagua miradi ya Maendeleo ikiwepo miradi  wa  ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Pinyinyi inayojengea Masusu kiasi cha Shilingi Milioni 580,ujenzi wa darasa Moja  shule ya msingi Masusu kiasi cha Milioni 20,na Nyumba ya Daktari Zahanati ya Pinyinyi inayojengwa na TASAF kiasi cha Milioni 89.

"Nawapongeza wananchi wa kijiji cha Masusu kwa kujitoa kuchangia mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Pinyinyi kiasi cha Shilingi Milioni 20 ikiwa ni sehemu ya kuchangia juhudi za Serikali ya Awamu ya sita ya Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassani" alisema Mhe Mwangwala

Dc Mwangwala kesho Septemba 19 2023 ataendelea na Ratiba yake ya kukagua miradi ya Maendeleo na Kusikiliza na kutatua Kero za wananchi.








Share To:

Post A Comment: