Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha kimeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM huku viongozi wa ngazi mbalimbali katika wilaya hiyo kuhakikisha ujenzi wa miradi ya Elimu na Afya inatekelezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa kutokana na kuelekezewa fedha nyingi na serikali katika miradi hiyo.

Akizungumza Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Arusha Timoth Sanga katika ziara ya Sekretarieti yake ya wilaya ya kukagua miradi mbalimbali ya sekta ya elimu na afya inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan 

"Tumeona katika Sekta ya Elimu ni bora kuikuza elimu yetu hapa nchini ili kuzidi kukuza vijana wetu na kuwa na taifa lenye wasomi wengi na wataalamu ambao watatusaidia kukuza taifa letu katika nyanja mbali mbali na Serikali imeamua kulitimiza hilo nimpongeze Rais wetu Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha katika sekta ya elimu ili kutimiza malengo ya ilani ya chama kwa wananchi". Alisema Sanga.

"Fedha hizi ni zawatanzania ambao wamejibana kwa matumizi yao na kulijenga taifa lao, niwaombe sana viongozi na wasimamizi kuwa waamifu ili kutimiza miradi hii kwa wakati na inapo timizwa ionekane thamani ya fedha kwenye kila mradi husika ili nchi ikaimarike na niwaombe watanzania wenzangu kulinda rasilimali hizi ili zidumu kwa maendeleo ya vizazi vyetu". Alisema Sanga.

Kwa upande wake Naibu Meya wa Jiji la Arusha Ndg, Abraham Mollel, Ameeleza kuwa wao kama Jiji la Arusha wamejipanga vyema kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na Serikali inakamilika kwa wakati na inatoa huduma kwa wananchi na kuweka wataalamu wa kutosha kuhakishasha huduma bora zinapatikana kwa wananchi.

"Tunaendelea kusimamia ipasavyo miradi mbali mbali inayoendelea kutekelezwa na serikali hasa katika sekta ya elimu tuaweka mabweni ya kutosha ili kuwasaidia wanafunzi wetu wasitembee umbali mrefu na kuweka miundo mbinu mingine mizuri ya kujisomea lengo letu ni tuwe na wasomi kwa maendeleo ya nchi". Alisema Mollel.

"Katika Sekta ya Afya tunaendelea kuweka vifaaa vya kisasa na watalamu zaidi ili kutoa huduma bora kwa wanchi wetu pa kuboresha makazi ya watumishi wetu pamoja na maslahi yao nimshukuru sana Rais Samia kwa kutoa fedha hizi za maendeleo ambapo zinaenda kutoa huduma kwa kila mtanzania". Aliongeza Mollel.

Hata hivy Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM ) wilaya ya Arusha Mjini Ndg, Mohamed Massud Mohamed ameeleza kuwa kwasasa siyo muda wa kusikiliza majungu na maneno ni wakati wa kufanya kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kama inavyo hitaji ipanai ya CCM na kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan.

"Sisi kama vijana tuliyopata nafasi ya kuaminiwa na Mhe, Rais tunapaswa kuhakikisha yale yote serikali inayofanya tuyasimamie kwa ukaribu na kushauri ili tusonge mbele kama taifa moja,maana lengo la Mhe, Rais ni kuhakikisha taifa linapata maendeleo". Alisema Mohamed.

Aidha pia Mohamed aliweza kuwashauri wanafunzi wazingatie elimu maana ndiyo mkombozi wa maisha yao na taifa kwa ujumla na kuwakanya vijana waliyopo mtaana wanao warubuni wasichana waliyopo masomoni na kuwahaidi kuwa serikali haita wafumbia macho kamwe endapo watakapo bainika kutenda makosa hayo.


Share To:

Post A Comment: