Mkurugenzi wa Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Rubby ijulikanayo Sendeu Agrovet Investment Limited, Gabriel Sendeu Laizer iliopo katika Kijiji cha Elesin'geta, Wilayani Longido mkoani Arusha (wa kwanza kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji hicho Akwelino Nikeni kadi ya gari aina ya Noah ikiwa ni zawadi kwa ajili ya kutambua utendaji kazi wake mzuri wakati wa uongozi wake. Tukio hilo limefanyika mwanzoni mwa wiki hii kijijini hapo.

Wananchi wa Kijiji cha  Elesin'geta  kilichopo katika kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha wametakiwa kuhakikisha wanatetea, kuhifadhi na kutunza ardhi yao kwa manufaa ya vizazi  vijavyo.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya Rubby ijulikanayo Sendeu Agrovet Investment Limited, Gabriel Sendeu Laizer
wakati akiongea mwanzoni mwa wiki hii katika sherehe za kumsimika mwenyekiti wa kijiji hicho mstaafu kuwa chifu wa ukoo wa Kipuyo (Legwanani) pamoja na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa uongozi wake.

Alisema kuwa ni vyema wananchi wa Longido wakaendelee kulinda na kuhifadhi vyema ardhi yao kwa ajili ya kuvihifadhia vizazi vijavyo kwani  iwapo wataitumia vibaya watasababisha watoto watakaozaliwa baadae kukosa ardhi ya kunitumia.

Laizer amewashauri pia vijana wa vijiji hivyo kufanya kazi kwa bidii, kuhifadhi na kutumia fedha ambazo wanazipata katika shughuli za maendeleo na sio kufanya anasa ili kuweza kujikwamua katika wimbo la umaskini na kuliongezea pato taifa.

"Niwasihi vijana ambao mpo hapa mnaofanya shughuli zenu ikiwemo za uchimbaji madini mtumie fedha hizo kwa maendeleo na sio mmalizie kwa wanawake pamoja na kunywa pombe," alisema Laizer.

Aidha alimshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuwapatia wananchi  wa wilaya hiyo maeneo kwa ajili ya kuchimba madini yaliyochangia kuwapatia vijana wengi ajira na kuwaondoa katika umaskini.

Pia alitoa shukrarani zake za pekee kwa Katibu Mkuu wa taifa wa (CCM) Comrade Daniel Chongolo pamoja na aliyekuwa Waziri wa Madini Dotto Biteko kwa kuwasaidia kwa kuwasaidia wananchi wa Longido kupewa maeneo kwa ajili ya kufanya kazi ya uchimbaji ambayo imesaidia sana vijana wengi kupata ajira.

Katika kutambua mchango wa Mwenyekiti mstaafu wa kijiji hicho Akwelino Nikeni katika kipindi cha uongozi wake aliweza kumkabidhi shukrani ya nyumba aliyomjengea pamoja na gari aina ya Noah.

Akitoa shukrani zake mwenyekiti mstaafu wa Kijiji hicho Akwelino Nikeni aliwashukuru sana wananchi kwa namna walivyotambua mchango wake aliyoutoa wa kusaidia jamii katika kipindi cha uongozi wake ambapo aliwahaidi kuendelea kuwapa ushirikiano hata katika kipindi ambacho hayupo katika uongozi.

"Nimshukuru Laizer kwa moyo wake wa kipekee wa kunipatia nyumba na gari ila ninawaahidi gari hili halitakuwa la matumizi yangu binafsi bali nitawasaidia wananchi wa Kijiji na kata pindi watakapokuwa na uhitaji wowote," alisema Nikeni.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli Isack Copriano aliwataka wananchi wa  wilaya ya Longido  kushirikiana kutunza udongo wa Tanzania maana hakuna hazina nyingine yoyote iliopo au watakao weza kupata zaidi  ya ardhi.

Alimpongeza Laizer kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema kuwa kazi kubwa ya Mzalendo ni kuajiri vijana bila kuwabagua huku akiwataka kuendelea kuonyesha Watanzania upendo na mshikamano
Share To:

Post A Comment: