Taasisi ya AGRI THAMANI kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (FAO), Wizara ya Kilimo pamoja na Serikali ya uingereza imekabidhi vibanda 35 kwa baba na mama ntilie katika soko la Kisutu jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kuongeza ufanisi katika kazi zao.


Kupitia programu ya Agri- Connect iliyoandaliwa na taasisi hiyo ya kiraia, wafanyabiashara hao wametakiwa kupika vyakula vya asili kwa kuzingatia usafi, ubora na bei nafuu.

Akizungumza katika halfa hiyo ya uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha ulaji unaofaa kwa kutumia vyakula vya asili hapa nchini, Kaimu Mkurugenzi wa Fao, Bw.Abebe Gabriel amesema watu wengi barani Afrika hula chakula ambacho hakina lishe bora.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Mobhare Matinyi ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema licha ya nchi kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100, lakini bado liko tatizo la utapiamlo kwa watoto ambalo ni matokeo ya lishe duni.

Amesema madhara mengine ni pamoja na watoto kuathirika kiakili na baadae kuwa na kizazi ambacho kina mchango mdogo kwa taifa.

Naye Meneja wa Agrithamani Bw.Theobald Sylvester amesema programu hiyo imeanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam na baadae itaenda katika Mikoa mingine ikiwemo Dodoma na Mbeya.

Katika hafla hiyo Mama Lishe walipika msosi wa Asilia na watu wakala ikiwa ni jitihada za kuhamasisha Matumizi ya vyakula Asilia.









Share To:

Post A Comment: