NA EMMANUEL MBATILO,


Mawaziri, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof Adolf Mkenda na Wizara ya Nchi, Ofisi  ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Angellah Kairuki  wamekutana  jijini Dar es salaam  na Kamati mbili za Kitaifa za Sera  ya Elimu na Maboresho ya Mitaala kwa lengo la kupokea wasilisho la  mahitaji ya utekelezaji wa Sera na Mitaala ya Elimu pendekezwa.

Wasilisho la pamoja limefanywa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maboresho ya Mitaala, Prof.Makenya Maboko aliyewasilisha juu ya mahitaji muhimu katika utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mitaala pendekezwa. 

Mawaziri hao kwa pamoja wameweza kupokea mapendekezo hayo na kutoa maelekezo mbalimbali ya kufanyiwa kazi kwa ajili ya kuboresha mapendekezo hayo kabla ya kupelekwa kwenye mamlaka za maamuzi.

Kikao hicho pia, kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne  Nombo na Naibu  Katibu Mkuu wa TAMISEMI-Elimu Dkt.Charles Msonde na Mwenyekiti wa Kamati ya Sera, Prof. Joseph Semboja.

Wengine waliohudhuria ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba pamoja na baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya TET na wajumbe wa Kamati ya Sera.

Share To:

Post A Comment: