Mtafiti wa haki za wanawake na watoto kutoka taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD)  na Citizen for Change C4C Bwana Mathias Mkude akizungumza kwenye kikao hicho leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga.

Na Hyasinta Ludovick, Mapuli Misalaba - Shinyanga

Wanawake ni kundi linalotajwa kukumbatia mifumo dume inayo sababisha kuendelea kwa vitendo vya ukatili katika jamii.

Hayo yamebainishwa na mtafiti wa haki za wanawake na watoto kutoka taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD)  na Citizen for Change C4C Bwana Mathias Mkude ,kwenye kikao cha kutoa matokeo ya utafiti wa kubaini visababishi vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mkude amesema Utafiti huo umebaini kuwa wanawake ni miongoni mwa watu wanaoendeleza  mifumo hiyo hasa katika ngazi ya familiya hali inayochangia kuendelea kuwepo kwa vitendo  vya ukatili .

“Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba mifumo isiyo rasmi inafanya kazi kwa nafasi ya kipee zaidi ya mifumo rasmi tulipita kwenye nyumba takribani zaidi ya elfu moja lakini katika hilo tulijaribu  kuangalia ni watu gani wanafuatwa zaidi pale watu wanapokutana na suala la ukatili kila kata walitajwa watu watatu na tulipata watu 54 na watu 50 walikuwa kwenye mfumo usiorasmi na wanne ndiyo walikuwa kwenye mfumo rasmi’.

“Tumegundua pia pamoja na kuwepo kwa matokeo ya ukatili wanawake kwa kiasi kikubwa ndiyo waendelezaji wa mifumo inayopelekea ukatili yaani mfumo dume hata mama kwenye ngazi ya familia anaona umuhimu wa mtoto wa kiume kuliko mtoto wa kike kwahiyo wanaamini kwamba ili uwe mwanaume lazima uwe mtu mwenye nguvu”.

“Lakini jamii iliweza kupendekeza njia saba ikiwemo kurudisha taratibu na kanuni  zile za  kimila zilikuwa zinawaweka pamoja kujadili pamoja na kutoa mambo ya pamoja lakini pia wamezungumza umuhimu wa kuwa na sheria ndogondogo ambazo zinazingatia katiba ya Nchi maana asilimia kubwa wanatumia sungusungu lakini hawa sungusungu wasipotengenezewa sheria za kuzifuata wakati mwingine inapelekea ukatili kwa watu wanaowapa adhabu”.amesema Mkude

Kwa upande wake mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga (WFT-Trust) Glory Mbia amesema utafiti huo umefanyika ndani ya  Miaka miwili (2) katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Afisa Miradi mwandamizi anaye shughulikia utetezi wa haki za watoto kutoka WFT Tanzania  Neema Msangi amebainisha malengo na majukumu ya mfuko huo katika kuyawezesha mashirika madogo na kwamba hatua hiyo ni njia ya kufikia malengo katika utetezi wa haki za wanawake na watoto.

“WFT ni mfuko wa ufadhiri ambao ulianzishwa toka mwama 2008 ukiwa na malengo makubwa ya kuangalia ufikiwaji wa haki za wanawake, wasichana na watoto kwa kuangalia upatikanaji wa rasilimali”.

“Lengo ni kuyafikia makundi au mashirika madogo ambayo yapo kwenye ngazi ya jamii ambao wanashindwa kufikia fund ambazo zipo juu tukaona tuwe na mfuko wa kuwawezesha mashirika ili kuweza kufikia malengo ya utetezi kwa wanawake, wasichana na watoto”amesema Neema.

“Tume hakikisha jamii inashiriki katika zoezi zima la utafiti huu lakini tumeweze kuona familia inakaa pamoja na watoto, wanawake wanasimama kwenye mikutano na kuongea kwa ujasili na kuchangia hoja ambazo zinaleta  maendelea kwenye jamii lakini pia atumweza kuona kunaongezeko la idadi ya kesi ambazo zimekuwa zikitolewa taarifa na taarifa hizi tumekuwa tukizifuatilia kwenye dawati la jinsia na watoto na kwa takwimu ambazo tumekuwa tukizipata ni kila mwaka kunakuwa na ongezeko la kesi hii ni kuonyesha kwamba jamii imenza kubadilika na kuona umuhimu wa kuripoti”.amesema Neema

Msimamzi wa Rasilimali,utafiti na mawasiliano wa Mfuko wa Rusuku wa Wanawake Tanzania(WFT-Trust),Carol Mango anasema zoezi la utafiti wa vitendo vya ukatili Halmshauri  ya wilaya ya Shinyanga lilikuwa ni muhimu ili kuelewa uhalisia wa tatizo la vitendo vya ukatili na kupata majibu yanayoweza kusaidia kutokomeza ukatili kwa kushirikisha  jamii yenyewe.

Utafiti huo ulifanyika kwa miaka miwili kwa kuhoji watu wapatao 1264 kwa makundi mbalimbali ndani ya Halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na shirika la Citizens  for Change.

Amesema utafiti huo uliona mambo 9 kwa yanayoweza kujadiliwa na wadau na kutoa maoni yao ambapo pia amesema zipo changamoto katika utafiti huo ikiwa ni kuchukua muda mrefu katika kupambana na ukatili ndani ya  jamii.

"Mambo 9 yalibainika ni pamoja na msaada wa mifumo isiyo rasmi una aminika na kufanya kazi,sheria za jamii   zina athiri mfumo rasmi,watu katika mfumo rasmi kuona ukatili ni watu wengine ,wanawake ni walinzi wa mila na destu katika jamii,wanawake na watoto wanahitaji mabadiliko,wawakilishi wa serikali ngazi ya kata hawashughuliko ukatili,kuelewa ukatili lazima uelewe nguvu ya mamlaka katika jamii na jamii inaweza kubadilika na kutegemeza mbinu zake wenyewe na wanaweke chanzo cha kuendeleza mila na desturi zinachochea ukatili”.amesema Mango

Akizungumza mgeni rasmi katika kikao hicho  cha kuhakiki na kujadili matokeo ya utafiti (Research Solution  Summit  in Shinyanga) masuala ya ukatili  uliyofanyika  katika  Halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga , Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje amewapongeza na kuwashukuru WFT – Trust kwa kutoa Ruzuku na kutekeleza miradi ya kupinga ukatili.

Amesema  katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga hali miradi hiyo imesaidia kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii huku akiomba kuendelea kutekeleza  miradi  ili kutokomeza kabisa ukatili.

Baadhi ya  wadau mbalimbali walioshiriki kikao hicho wamepokea huku wakiipongeza WFT – Trust kwa hatua nzuri waliyofikia katika utafiti Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo wameahidi kuendelea kuunga mkono jitihada hizo ili kutokomeza mila na destiri kandamizi zilizopo kwenye jamii.

Kikao cha kutoa matokeo ya utafiti wa kubaini visababishi vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kilichoendeshwa na taasisi ya Citizen for Change kwa ufadhili wa mfuko wa ruzuku wa wanawake Tanzania WFT – Trust kimefanyika kwenye ukumbi wa Karena Hoteli uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Mtafiti wa haki za wanawake na watoto kutoka taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD)  na Citizen for Change C4C Bwana Mathias Mkude akizungumza kwenye kikao hicho leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye kikao hicho leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye kikao hicho leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga.

 Kikao cha kutoa matokeo ya utafiti wa kubaini visababishi vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kilichoratibiwa na WFT –Trust kwa kushirikiana na C4C kiliendelea leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga.






Share To:

Misalaba

Post A Comment: