Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa majaliwa azindua mradi wa maji wa kitama Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara. Mradi huo umegharimu thamani ya shilingi Milioni 798.7.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb) katika hafla hiyo amesema kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa tank la lita laki 100, ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 20.1 , ujenzi wa vioski 10 vya kuchotea maji
Pia Mhe. Mahundi ameeleza kuwa Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika miji 28 ambapo kwa Wilaya ya Tandahimba mkandarasi ameshaanza utekelezaji wa mradi wa Makonde kwa gharama ya shilingi Bilioni 84 ambapo mpaka sasa Mkandarasi amepewa shilingi Bilioni 12 kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo.
Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu amepongeza Wizara ya Maji kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji Nchini na kusisitiza kuwa wananchi waendelea kulinda miundombinu ya maji pamoja na kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ili miradi hii inayotekelezwa kwa Awamu ya Sita iwe endelevu.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe. Ahmed Katani Katani ameishukru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mingi ndani ya jimbo lake ukiwepo mradi wa miji 28 wa Makonde ambapo kukamilika kwako kutaboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Tandahimba
Post A Comment: