Na DENIS CHAMBI, TANGA.
SERIKALI
imewaagiza wakandarasi na wawekezaji wa kimataifa wanaoutekeleza miradi
mbalimbali ya kimkakati hapa nchini kuhakikisha kuwa wanazingatia usawa
wa kijinsia katika utoaji wa ajira kwenye shughuli mbalimbali
wanazozisimamia ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele cha wazawa wakiwemo
wanawake na makundi maalum.
Rai
hiyo imetolewa mkoani Tanga na waziri wa jinsia wanawake na makundi
maalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akimwakilisha waziri mkuu Kassim
Majaliwa katika kufungua kongamano la wanawake na manunuzi
lililoandaliwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Mhandishi
Mwanaisha Ulenge ambapoa amesisitiza kuwa ni lazima ushiriki wa jamii
katika utekelezaji wa miradi hiyo upewe kipaumbele.
Aidha
taasisi zote zinazotekeleza na kusimamia miradi ya kimkakati
zihakikishe kuwa zinawasilisha taarifa za utekelezaji wa ushiriki wa
watanzania katika ofisi ya waziri mkuu kupitia Baraza la Taifa la
uwezeshaji wanawake kiuchumi ili kuiwezesha nchi kupata na kupima
thamani inayobaki kwenye uchumi wa nchi.
"Waziri
mkuu anasisitiza kuwa wawekezaji na wakandarasi wa maswala ya
kimataifa wa maswala ya kiuchumi wahakikishe kuwa maswala ya kujengea
ujuzi kwa watanzania uhaulishaji wa teknolojia na ushiriki wa jamii
kwenye eneo la uwekezaji yanapewa kipaumbele na taasisi zote
zinazotekeleza mradi wa kimkakati ziwasilishe taarifa katika ofisi ya
waziri mkuu kupitia baraza la Taifa la uwezeshaji ili kutuwezesha nchi
kupima thamani ya kutokana na ushiriki wa watanzania alisema Gwajima
"Watanzania
hususan wanawake wapewe kipaumbele katika ajira na manunuzi ya umma
katika miradi yote ya kimkakati inayotekelezwa nchini na kwenye fursa
za biashara kupitia ujuzi walio nao na bidhaa ili kukidhi viwango"
"Lakini
pia waziri mkuu anasisitiza ufwatiliaji na tathmini kuhusu
ushirikishwaji wa watanzania katika miradi ya kimkakati uendeleee
kufanyika ili serikali iweze kuchukua hatua stahiki kuhusu changamoto
zinazojiyltokeza mara kwa mara ili ushiriki wa watanzania uweze kuwa
wenye tija na manufaa kwa ujumla na mimi nasema taarifa zote
tutazifwatilia na miradi itekeleze uwiano wa kijinsia ili kutimiza
adhima ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya uwezeshaji wanawake
kiuchumi" alisisitiza Dkt. Gwajima.
Dkt
Gwajima amabaye pia alizindua taasisi ya Ng'arisha Maisha
iliyoanzishwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Mwanaisha Ulenge
amewataka wanawake kujiunga na kutumia vyema mabaraza ya uwezeshaji
wanawake kiuchumi yaliyopo ili kuweza kuwasaidia katika maswala
mbalimbali yanayowahusu ikiwemo ya kiuchumi huku akizitaka taasisi za
kifedha kuendelea kuwewezesha mikopo wananchi ili kuweze kujikwamua
kiuchumi .
Awali
akizungumza mkurugenzi wa taasisi ya Ngarisha maisha Foundation
Mhandisi Mwanaisha Ulenge amesema kupitia taasisi hiyo isiyokuwa ya
kiserikali wamedhamiria kuwainua wananchi hususan wanawake katika
kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta za kilimo uvuvi na biashara sambamba
na kuunga mkono juhudi zote za serikali zinazolenga kuwaletea maendeleo
wananchi.
"Taasisi ya
Ng'arisha Maisha foundation ni ya kitaifa isiyokuwa ya kiserikali
inayolenga kuwainua wananchi kiuchumi hususan wanawake , taasisia
imeleta mafunzo hayo kwa lengo la kuunga mkono jiyihada za serikali
katika kuwaleta watanzania maendeleo, taasisi ya NMF imedhamiria
kuunga mkono jitihada za serikali katika kutatua changamoto za makundi
maalum wakiwemo wanawake, na kuhakikisha mipango ya serikali ya
kimaendeleo inawafikia walengwa wakiwemo wanawake"
"Taasisi
ya Ng'arisha Maisha foundation 'NMF' itasisimamia ugawaji wa mbegu
bora za Alizeti kwa wakulima hususan wanawake na kuwapelekea wananachi
kuachana na kilimo cha asili badala yake kujiingiza kwenye kilimo cha
kisasa, na taasisi itaendelea kugawa mbegu bora kwa wananachi hususan
wanawake, ni matumain yetu barabara ya Handeni kwenda Kibirashi wakulima
wa zao la Alizeti wataweza kunufaika nayo".
"Pamoja
na kuwezesha mbegu kwa wananch nimewezesha vijana kupata elimu katika
vyuo vya kati pamoja na kuwezesha vifaa tiba kwa watoto njiti. nipo
kwenye mchakayo wa kuwezeaha miguu bandia 100 kwa wahitaji, kuhusu
uvuvi bado wanawake walionufaika ni wachache sana, taasisis yeyu
itaweka mipango zaidi kuhakikisha wanawake wengi zaidi wananufaika
tunaomba serikali iwezeshe vifaa ili wanawake waweze kunufaika na uchumi
wa bluu".
Kwa upande
wake waziri wa afya na mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Mhandishi Mwanaisha
Ulenge kwa kuja wazo la kuanzisha taasisi ya Ng'arisha Maisha foundation
ambayo inakwenda kugusa Maisha ya wananchi moja kwa moja hususan
wanawake katika nyanja mbalimbali.
"Tunashukuru
sana mheshimiwa Ulenge kwa kuthubutu na tutaendelea kufanya kazi pamoja
kwaajili ya manufaa ya wanawake wa mkoa wa Tanga hususan kupitia
taasisi hii uliyoianzisha lakin Jambo la kusistiza ni kwamba uchumi
unaendana na afya bora kwahiyo pia tutazungumza na maswala ya saratani
hususan saratan ya kizazi, matiti tuweze kupata matibabu" alisema Ummy.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga na mkurugenzi wa taasisi ya Ng'arisha Maisha Foundation Mhandisi Mwanaisha Ulenge akizungumza katika kongamano la wanawake na manunuzi ya Umma(Daraja Comference )lililowakutanisha wanawake zaidi ya 1000 wa mkoa wa Tanga kujadii fursa mbalimbali ikiwemo za uchumi.
Post A Comment: