Serikali itaendelea kufuatilia na kuhimiza ujenzi wa kampasi ya Chuo Kikuu cha Agha Khan mkoani Arusha


Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Jijini Arusha alipotembelea eneo litakalojengwa Kampasi hiyo.

Prof. Mkenda ameongeza kuwa Serikali itaendelea kufuatilia ujenzi wa kampasi hiyo na kuagiza iwe ni kituo cha umahiri cha chuo hicho kwa Afrika Mashariki.

1000236680

"Kazi yetu sisi kama serikali ni kufuatilia, kuhimiza na kuangalia changamoto zilizopo tusaidie kuzitatua kampasi hii ijengwe na kiwe kituo cha umahiri cha chuo hicho kwa Afrika Mashariki" ameongeza Prof. Mkenda.

Waziri huyo ameongeza kuwa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa imefungua nchi ni pamoja na kuwa na vyuo vikuu ambavyo watu wetu na wa kutoka nje watavitumia katika kupata ujuzi na maarifa.

1000236659

Ameongeza kuwa Taasisi ya Agha Khan inatambulika kwa kutoa huduma bora katika maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu na kwamba ni mategemo ya serikali kuwa kampasi hiyo itakuwa bora katika ukanda wa Afrika Mashariki.




Ameelezea historia ya kupelekwa Arusha kwa Kampasi hiyo, Prof. Mkenda amesema Rais wa Awumu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ndio aliomba kwa Mtukufu Agha Khan kujenga Kampasi hiyo Mkoani Arusha ili iwe karibu na Makao Makuu ya Taasisi hiyo yaliyopo nchini Kenya

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Agha Khan Eunice Pallagyo amesema kuwa pamoja na kwamba Kampasi hiyo bado haijajengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo lakini shughuli za utafiti mbalimbali unaendelea katika eneo hilo.
1000236651
1000236684
1000236665
1000236679

Share To:

Post A Comment: