Basi la Mining Nice linalofanya safari zake kati ya Mtwara na Morogoro likiwa limepinduka mkoani Lindi. Katika ajali hiyo hakuna vifo vilivyotokea isipokuwa abiria kujeruhiwa.
................................................... 

Na Said Hamdani, LINDI.

 

ABIRIA 40 waliokuwa wanasafiri na Basi la Kampuni ya Maning Nice kutoka mkoani Mtwara kwenda Morogoro wamenusulika kiifo kufuatia gari walilokuwa wakisafiria kuacha barabara na kupinduka.

Kwa mujibu wa mashuhuda na abiria waliokuwa wanasafiri na basi hilo walisema ajali hiyo,imetokea mtaa wa Likong'o Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, August 23 majira ya saa 4:30 asubuhi.

Wakizungumza na mwandishi wa habari  hizo aliyetembelea eneo la ajali na Hosptali ya mkoa you,Sokoine, baadhi ya Abiria Armani Nakuwa,Said Ng'ombo na Cosmas Milanzi wametaja Chanzo cha Ajali ni kujaribu kuipita Lori la kubeba mizigo la Kampuni ya Dangote

Abiria hao waliokuwa wanasafiri na basi lenye namba za usajili T 896 DUY kutoka Mtwara kwenda Morogoro walisema wamepata ajali kufuatia dereva wa basi lao kulipita lori lililokuwa limesimama eneo lenye kona mlima  Likong'o.

Walisema lori hilo lilikuwa limesimama mlimani baada ya kuharibika,hiyo dereva wao wakati analipita mbele kulikuwa na pikipiki na magari mengine yakielekea mikoa ya kusini.

"Mbele yetu kulikuwa na Lori la Dangote limeharibika,wakati analipita tukakutana na Pikipiki na gari nyingine katika kuzikwepa basi letu likapoteza mwelekeo" walisema abiria hao.

Abiria hao wamemsifu dereva wa basi kuendesha mwendo ambao haukuwa na kasi na kuweza kupata nusura ya kutopoteza maisha.

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo Said Chotani na Mwanaisha Ally wamedai dereva wa pikipiki alikuwa mbishi  kulipisha basi hilo la Maning Nice licha kupigiwa honi mara kadhaa.

Mashuhuda hao walisema kulikuwa na mwendesha pikipiki hataki kupisha dereva wa  basi alipojaribu kumkwepa ndipo likakosa mwelekeo kutokana na utelezi uliochangiwa na mvua iliyokuwa ikinyesha.

Pia,wameeleza baadhi ya  abiria wamejeruhiwa maeneo ya mikono na miguu ambapo walipelekwa  Hosptali ya Mkoa Sokoine kwa matibabu.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hosptali ya Sokoine Baraka Mshamu amekiri kupokea majeruhi 16 kati yao wanaume (11) na wanawake watano akiwemo mtoto mmoja ambaye akumtaja  jinsi yake.

Amesema kati ya abiria hao wawili wameumia mkono na mguu wa kulia na kupelekwa chumba cha upasuwaji kwa matibabu na waliobaki wamepata majeraha madogo madogo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pili Mande alipotafutwa kupitia simu yake ya mklononi ili kupata kauli yake hakuweza kupatikana .

Mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri na basi hilo, Said Ng'ombo akielezea jinsi ilivyotokea ajali hiyo.


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: