Na; Moreen Rojas, Dodoma.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ernest Ibenzi amesema watumishi wa hospitali hiyo wanaendelea kupata mafunzo sehemu mbalimbali ikiwemo nje ya nchi.


Akizungumza leo jijini Dodoma, Dkt. Ibenzi amesema mafunzo yanawasaidia kujua teknolojia mpya ili kuendeleza juhudi za kuboresha huduma hospitalini hapo.


"Mkiona hospitalini pamejaa wanafunzi msishangae, tuna wanafunzi wanaokuja kwa mafunzo, wale ni madaktari wenzetu, wale ni wauguzi wenzetu, tunawafunza kutibu kwa vitendo, hatuwaruhusu kutibu wakiwa peke yao," ameeleza Dkt. Ibenzi.


Aidha, Daktari huyo amearifu kwamba hospitali yao inaendelea kutatua changamoto mbalimbali ili wananchi wapate huduma bora.


"Tunataka wateja wetu wapate huduma bila changamoto yoyote, dawa zote tunazo hospitali, hutokea bahati mbaya dawa hamna labda inapatikana Kenya, huwa tunawapa wagonjwa siku mbili waje wachukue," amesema Dkt. Ibenzi.



Kuhusu changamoto ya msongamano wa wagonjwa kwenye wodi ya watoto ambapo watoto hulazwa wawiliwawili katika kila kitanda, Dkt. Ibenzi ameeleza kwamba tatizo hilo litakwisha ndani ya wiki mbili zijazo.


Aidha amesema kuwa vyumba vya upasuaji 12 na kufanya upasuaji hadi wagonjwa 70 kufanya upasuaji masaa 24 ili kupunguza msongamano wa wagonjwa huku kwa siku wakiwa wanapokea wagonjwa 1,500.

Aidha ameongeza kuwa katika wagonjwa ambao wametibiwa kwa muda mfupi ni katika watu wanaovunjika miguu na mikono kuweza kuendelea na shughuli zao ndani ya wiki moja hivyo wameendelea kuboresha huduma zao kwenye nyanja mbalimbali.


"Kuhusu changamoto ya wagonjwa kuzikwa na jiji ni kutokana na kukaa hospitali muda mrefu bila ndugu au wengine kupata ajali na kufikishwa hospitali bila kitambulisho chochote huku ikiwa baadhi ya viungo vimesagika na hii inapelekea kushindwa kupata ndugu zake hivyo kama hospitali wanachukua jukumu la kuwa ndugu ili kumstiri mgonjwa husika"Amesema Dkt.Ibenzi


Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 wanategemea kama hospitali kukusanya bilioni 24 ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ikiwa ni pamoja na vifaa tiba ili kufikia asilimia 99% za utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.






MWISHO.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: