Wakazi, wa Kata za Ndala, Masekelo na Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa Barabara kipande cha kuelekea katika hospital ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ili kuwaepusha na athari ya vumbi kali linalotimuka.

Kwa nyakati tofauti wamezungumza watumiaji wa Barabara hiyo, madereva wa magari,Bajaji, waendesha Baiskeli, pikipiki pamoja na wananchi wanaoishi kando kando ya Barabara hiyo kipande cha kata za Ndala,Masekelo,na Mwawaza ambao wamelalamikia vumbi kali linalotimuka na kutishia usalama wa afya zao

Wameiomba serikali kutimiza ahadi yake ya kukamilisha ujenzi wa Barabara hiyo kwa kiwango cha lami ili kuwaepusha na madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na Vumbi kali linalotimuka mchana na usiku

Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA Wilaya ya Shinyanga,  Injinia Samson Pamphil amesema Barabara hiyo ipo kwenye mpango wa ukamilishaji  kwa kiwango cha lami kama ilivyoahidiwa na serikali  ambapo amewaomba wananchi kuwa na subira kwani kinachosubiriwa ni fedha kutoka serikali kuu.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: