Na Moreen Rojas,Dodoma.

Wananchi washauriwa kutumia mbegu bora ili kujiongezea kipato na kwenda na kasi ya uchumi wa kati ambapo kilimo ni uti wa mgongo wa nchi.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuthibiti Ubora wa mbegu Tanzania(TOSCI) Patrick Ngwediagi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari jijini Dodoma.


Aidha ameongeza kuwa takribani Tani 1 na zaidi zimeuzwa nje ya nchi ambapo mbegu zilizouzwa ni mahindi na mbogamboga na mpka sasa kesi 5 za mbegu feki zimepelekwa mahakamani.


"Ni kweli tumepambana na uwepo wa mbegu feki na miaka saba iliyopita kila mbunge alikuwa akisimama bungeni anazungumzia suala hili,lakini tumejitahidi kuhakikisha tunadhibiti mbegu feki,hivyo kwa sasahivi hakuna changamoto hiyo lakini huko nyuma tulipokea malalamiko takwimu za kipindi cha nyuma na sasahivi ni tofauti hivyo suala la mbegu feki limeweza kushughulikiwa na wananchi ukiwauliza kuhusu mbegu feki anakwambia nimeweza kugundua mbegu feki sababu haina nembo ya TOSCI".



Aidha amesema kuwa Tani 1 na zaidi zimeuzwa nje ya nchi ambapo ni mahindi na mbogamboga huku kesi 5 za mbegu feki zimepelekwa mahakamani.


Aidha ameongeza kuwa huwezi kufanya biashara yoyote ya mbegu bila kuzajiliwa na TOSCI ikiwa ni pamoja na kukagua mashamba yote yanayozalisha mbegu pia kukagua maduka na maghala.


TOSCI imefanikiwa kuongeza uwezo wa kusimamia ubora wa mbegu pamoja na kuwashawishi wazalishaji wa mbegu kuzalisha mbegu hapa nchini mbegu hizo ni pamoja na mahindi,mpunga,mtama,alizeti,mbegu za mboga,peas,malisho,maharage,pamba,choroko,mbaazi,karanga,ufuta,ngano,kunde,njugu mawe,ulezi,tumbaku,pamoja na maharage ya soya.



Sanjari na hayo TOSCI imeimarisha na kuanzisha ofisi za kanda ili kutoa huduma zake kwa wadau kwa karibu zaidi,ofisi za kanda ya ziwa na kanda ya kusini zimefunguliwa wakati ofisi za kanda ya kaskazini na nyanda za juu kusini zimeboreshwa majengo na pia kupata watumishi zaidi.


Katika mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya shilingi 10,650,420,232.00 zilitegwa kwa ajili ya matumizi ya mishahara pamoja na matumizi ya kawaida ya maendeleo.


Jukumu kubwa la TOSCI ni kusimamia shughuli za uzalishaji wa mbegu na biashara ya mbegu ili kuwahakikishia wakulima na wadau wengine wanazouziwa zikiwa na lebo ya ubora ya TOSCI ni mbegu sahihi kwa matumizi.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: