Julieth Ngarabali ,Kibaha
Wajawazito na watoto wa umri wa miaka 0 mpaka nane katika kata ya Misugusugu mjini Kibaha wameondokana na adha ya kusafiri umbali wa zaidii ya km 20 kufuta huduma za afya huko Mlandizi Kibaha Vijijini kufuatia kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa zahanati ya kisasa ya Saeni na kuanza kutoa huduma zote ikiwemo ya afya ya uzazi.
Wajawazito hao ni miongoni mwa Wananchi takribani 14,000 wanaoishi kwenye mitaa mitatu ya Saeni, Zogowale na Jonung"ha katika kata ya Misugusugu mjini Kibaha ambao awali walikabiliwa na changamoto ya kutembelea umbali mrefu kufuata huduma za afya
Akizindua kuanza huduma za afya katika zahanati ya Saeni ,Mbunge jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema kuanza kwa huduma hizo ni jitihada za Wananchi wa maeneo hayo kujitolea nguvu zao, yeye mwenyewe, halmashauri na Serikali
Koka amesema wananchi walipochoshwa na adha ya kutembea umbali mrefu walitafuta eneo la ujenzi wa mradi huo ambapo katika kuwaunga mkono alichangia sh. 6.5 Milioni kwa ajili ya kununua mifuko ya saruji ya kuanzia ujenzi huo na wadau wengine wakaunga jitihada hizo.
" Mnakumbuka wakati nilipoomba ridhaa ya kuwa Mbunge wenu mliniambia mna shida ya maji, barabara na zahanati niliwapigia magoti kuwaomba kuwa tutazitatua na kweli tumeshirikiana sisi ,halmashauri na Serikali ya CCM leo tumekamilisha vyote maana ,zahanati ndio hii tumeifungua ni mkombozi mkubwa sana hapa" amesema Koka
Koka alibainisha lengo lake kubwa ni kuwatumikia wananchi hivyo atahakikisha anaendelea kushirikiana nao jimboni humo kwenye sekta zote ili waweze kuondokana na kero ambazo wamekuwa wakizipata.
Awali mganga mfawidhi wa halmashauri ya mji Kibaha Peter Nsanya amesema mradi wa Ujenzi zahanati hiyo mpaka kukamilika umegharimu sh. 181. milioni zilizotokana na nguvu za wananchi,mbunge huyo, halmashauri na Serikali kuu.
," mradi wa ujenzi huo utaweza kusaidia zaidi hasa kwa Upande kwa huduma za mama na mtoto ambao walikuwa wanapata shida ya kusafiri mbali kuzifuata huko Mlandizi , hata hivyo bado upo upungufu wa viti " amesema Dk. Nsanya
Aidha Diwani wa kata ya Misugusugu Upendo Ngonyani amemshukuru Mbunge Koka kwa namna anavyoshirikiana na Wananchi kuzitatua changamoto zilizopo na piai kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo
Baadhi ya wakazi wa mitaa hiyo wameshukuru mradii huo kuanza kazi kwani itaongeza chachu ya wajawazito wengi kuanza kliniki mapema, kupata elimu ya lishe,kupata kinga ya maradhi mbalimbali ikiwemo saratan ya mlango wa uzazi na pia wengine kupata tiba kwa wakati
Post A Comment: