NA DENIS CHAMBI.
MKUU wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameziagiza halmashauri zote mkoani hapa kuendelea kutoa anuani za makazi katika maeneo ambayo bado pamoja na kuweka vibao vinavyoelekeza maeneo mabalimbali ikiwa ni maelekezo ya serikali katika kuhakisha huduma za kijamii zinaendelea kutolewa kwa urahisi kama ilivyokusudiwa.
Kindamba
ametoa maagizo hayo leo wakati akifungua mafunzo ya matokeo ya sensa ya
watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi , watendaji, wawakilishi wa
vyama vya siasa na makundi maalum wa mkoa na halmashauri ya jiji la
Tanga ambapo amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya wananchi
wakieleza kuwa bado hawajapata anuani za makazi na vibao vilivyokuwa
vimewekwa viking'olewa.
"Kumekuwa
na changamoto katika utekelezaji wa anuani za makazi na wapo ambao
wamesema bado hawajapatiwa anuani zao, wengine wakisema kuwa vibao
vimeng'olewa hivyo niagize kuendelea kuweka vibao kwa maana ya alama
ambazo zinatambulisha mitaa yao kama mnavyofahamh hili ni zoezi endelevu
kwahiyo uongozi wa halmashauri na majiji yetu ni lazima kyhakikisha
zoezi hili linaendelea kwa kasi ili kutambulika na kufikika kirahisi"
"Tuachane
na mazoea ya kizamani maendeleo ya teknolojia yameongezeka na
yamekuwa yakibadilika badilika sana kwahiyo ni lazima tukubaliane
hatuweze kwenda kwa namna hiyo." alisema Kindamba.
Alisema
kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 idadi
ya watu mkoani Tanga imeongezeka kutoka 2, 45, 205 kwa mwaka 2012 na
sasa imefikia 2, 615, 557 kwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la watu 570
,392.
"Kwa kujibu wa
takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 idadi ya watu mkoani
Tanga imeongezeka kutoka milion mbili elfu atobaini na tano mia mbili
na tano kwa mwaka 2012 hafi kufikia milion mbili laki sita elfu kumi na
tano mia tano hamsini na saba sawa na ongezeko la watu laki tano elfu
sabini mia tatu tisini na mbili kwa mwaka 2022" alisema Kindamba
Awali
akizungumza meneja takwimu wa mkoa wa Tanga Tonny Manjota amesema
kuwa hadi sasa ripoti kumi zimekamilishwa kulingana na makundi
mbalimbali kwa kuonyesha matokeo ya sensa ya mwaka 2022 ambayo
yatasaidia wataalam katika mpango wa maendeleo ya Taifa.
Alisema
sensa ya watu na makazi iliyofanyika kitaifa mwaka 2022 ambayo ni ya 6
hapa nchini imekuwa ya tofauti na zilizopita ikiwa imeanza na
uhamasishaji pamoja na uyoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa
kushiriki kikamilifu ambapo kumekuwa na mayokeo chanya mpaka mwisho wa
zoezi hilo.
Kulingana na
sensa ya mwaka ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 matokeo
yameonyesha kuwa watoto tegemezi chini ya miaka 15 kitaifa imekuwa
ikipungua kutoka 42.3 hadi 40.8 na mkoa wenye watoto wachache ni Dar es
salam.

Baadhi ya viongozi , watendaji, wawakilishi wa vyama vya siasa na makundi maalum wa mkoa na halmashauri ya jiji la Tanga wakiwa katika mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yaliyofanyika Augost 16,2023 kwenye ukumbi wa Legal Naivera.
Post A Comment: