Na Denis Chambi, Tanga.

WATANZANIA wametakiwa kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara badala ya kungoja mpaka waugue kwani,  itawasababishia gharama  kubwa za kujitibia.

Rai hiyo imetolewa na waziri wa afya na mbunge wa jimbo la Tanga Ummy Mwalimu wakati akizindua kambi ya upimaji wa magonjwa mbalimbali bure inayoendeshwa kwasiku tano na taasisi ya Afya Check kwenye viwanja vya Usagara mkoani T    anga ambapo zaidi ya wananchi 1000 wamejitokeza kufanya vipimo vinavyotolewa bure.

Kambi hiyo ambayo i medhaminiwa na benk ya crdb itahusisha upimaji wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoyakuambukiza ambapo mara baada ya kugundulika mgonjwa atapatiwa dawa na kwale watakaokuwa na ulazima wakufanyiwa upasuaji watapewa rufaa.

Akifungua rasmi kambi hiyo itakayochukua siku tano jijini Tanga leo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema kwamba  kumezoeleka tabia  kwa watu wengi  kutopima afya zao  kwa kipindi cha  muda mrefu mpaka wapatapo maradhi.

Alisema  mazoea hayo ni mabaya kwani  yamewasababishia watu wengi  kuingia gharama za matibabu wanapougua ambapo wakati mwingine hushindwa kulipa na hivyo kuwaingiza katika matatizo ya kutopata matibabu yanayostahili.

Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini,  alibainisha kuwa ulaji wa aina ya  vyakula unaweza ukawa ni sababu ya kupata maradhi.

“ Tumezoea kula vyakula vyenye mafuta mengi tukiamini hicho ndicho chakula bora kumbe tunajichimbia wenyewe kaburi la kifo kutokana na kuzidisha mafuta ambayo ndiyo kisababishi cha madhara ya afya yetu”, alitahadharisha.

Waziri alitaja baadhi ya vyakula vinavyotumiwa na watu  kwa wingi tena kwa mazoea kuwa ni pamoja na sukari au chumvi iliyopitiliza.

Aliwataka Watanzania  kufanya mazoezi ya miili ikiwa pamoja na kutembea, kukimbia au hata kuzunguka nyumba unayoishi mara kadhaa ili mradi utokwe jasho.

Aliwahakikishia wakazi wa Tanga kuwa ataendelea kuwatumikia kwa moyo mkunjufu ikiwa ni pamoja na kushirikiana na taasisi/mashirika ya ndani na nje ili kuleta huduma mbalimbali zihusuzo afya na matibabu.

Mratibu wa Taasisi ya AfyaCheck, Dr. Isack Maro alisema katika siku tano watakazoendesha zoezi hilo, mkazo mkubwa utawekwa katika magonjwa yasiyoambukiza ambayo ni pamoja na magonjwa ya Pressure na Kisukari akibainisha kuwa kwa siku ya kwanza zaidi ya wananchi 1000 wamejitokeza . 

Alisema amevutiwa sana na mwitikio wa watu katika zoezi hilo kwani makisio ya awali ilikuwa angalau watu 400 wangehusika, lakini kwa leo (jana) pekee waliojiorodhesha wamefikia watu 1400.

“Kwa hali hiyo inaonesha huenda idadi ya watu watakaohudumiwa wakafikia zaidi ya 5,000.   

Akitoa nasaha zake kwenye hadhara hiyo, Samson Keenja,  Meneja Mwandamizi wa CRDB, Kanda ya Kaskazini alisema benki yake iko tayari kushirikiana katika majukumu yahusuyo utoaji huduma kwa jamii kwani ndilo lengo kubwa la taasisi yake.

Alimhakikishia Waziri kwamba CRDB itaendelea kutoa msaada kwa jamii kila itakapoombwa.

Alisema katika jitihada hizo za kusaidia jamii, CRDB,  iliendesha CRDB International Marathon iliyokusanya jumla ya shs.470 milioni ambazo zilipelekwa kwa shughuli za kusaidia jamii.

Mratibu wa Afya Check Dkt Issack Maro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma wanaozitoqa katika kambi hiyo iliyozinduliwa na waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo Augost 21,2023.

Meneja Mwandamizi wa benki ya CRDB Samson Keenja ambao ni wadhamini wakuu wa kambi hiyo inayofanyika mkoani Tanga kwa muda wa siku tano, akizungumza na waadhishi wa habari kuhusu ushiriki wao katika kuunga mkono juhudi za serikali kupitia sekta ya afya.

Baadhi ya wananchi mbalimbali wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye kambi ya upimaji wa afya  bure inayotolewa na taasisi ya Afya Check kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge wa jimbo la Tanga Ummy  Mwalimu.
 

                                                                                                                                                                                                                     

Share To:

Post A Comment: