Na John Walter-Manyara

Neema hiyo inatokana na Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga kuzindua mfumo wa stakabadhi ghalani kwa mazao ya Mbaazi na Vitunguu Saumu unaoanza kutumika sasa.

Aidha amewaasa wakulima mkoani humo kujiunga na mfumo huo utakaowasaidia  kunufaika na kilimo chao kwa kuuza mazao kwa bei nzuri kupitia maghala yaliyowekwa na vyama vya ushirika.

Aidha Sendiga amewasihi wafanyabiashara kuhakikisha wanaweka chapa ya mkoa wa Manyara kwenye mazao yote yanayouzwa kama alama ya kuutambulisha mkoa  pamoja na Tanzania kimataifa.

"Ni nia nyingine ya kufungua milango kimahusiano na inasaidia kulinda rasilimali tulizonazo kwani ununuaji wa kwetu sisi unapeleka hizi bidhaa zikiwa bidhaa halali kutoka Tanzania na makampuni ya nje yanayotaka kununua lazima yafanye ubia na makampuni ya ndani na nitahitaji chapa za bidhaa zao kusomeka Manyara Tanzania"

Ameongeza kuwa mara nyingi changamoto za usafiri husababisha hasara kwa wafanyabiashara kutokana na miundombinu mibovu ya barabara inayopelekea magari kuharibika mara kwa mara na mazao kupoteza ubora yanapofika kwa wanunuzi jambo linalosababisha kuuzwa kwa bei ndogo na kuharibu soko kimataifa, hivyo mfumo wa stakabadhi ghalani utawapunguzia wafanyabiashara adha ya kwenda vijijini kununua mazao na badale yake watanunua moja kwa moja kwenye maghala ya vyama vya ushirika kwa bei nzuri itayompa faida mkulima.

"Gari zinanasa huko hla yote inaishia kwenye kumlipa kwenye gari ulilokodi ili mzigo ufike msimu unaisha unakuta umepata hasara umekodi gari halina uhakika limetengenezwa njian siku Tano oil yote imehamia kwenye mazao na huwezi kuuza unakuwa umekula hasara lakini kwa mfumo huu mnunuzi hutoingia Chaka hata moja"

Kwa upande wake kaimu mtendaji wa bodi ya usimamizi stakabadhi ghalani  Asangye Bangu amesema mfumo wa Stakabadhi Ghalani unasaidia wakulima  kupata tija ya kazi wanayoifanya kwa kuhakikishiwa bei nzuri katika mazao yao na kuongeza ushindani sokoni.

Kutokana na shughuli za uzimaji wa mwenge mwaka huu zitakuwa mkoani Manyara, Bangu ameuomba uongozi wa mkoa kuuzungumzia mfumo huo namna ulivyowasaidia wananchi.

Kwa upande wa katibu tawala wa mkoa wa Manyara Carolina mthapula amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwemo mfumo huo wa stakabadhi ghalani.

Mkoa wa Manyara ni mkoa wa tatu ulioanza kutumia mfumo huo katika manunuzi ya mazao ya kilimo hasa mazao ya kimkakati ya vitunguu swaumu na mbaazi.

Wafanyabiashara, viongozi wa vyama vya ushirika AMCOS, Mawakala wa ununuzi wa mazao wameupokea kwa mikono miwili mfumo huo wakiamini utakuwa na tija kwao.


Share To:

Post A Comment: