Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amezindua Mradi wa maji Endirima/Lumbwa ambao unaonufaisha jumla ya wakazi wapatao elfu 7 wa vitongoji  vya Lumbwa, Elmanyara, Meirugoi na Endirima

Wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mhe.Mahundi amewasisitizia wananchi kuwa ni muda sasa wa kutunza na kulinda miundombinu ya maji ili mradi huo uwe endelevu ambapo kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa tank la lita 135,000, ulazaji wa bomba kilomita 20.7, ujenzi wa vituo vinne(4) pamoja na ujenzi wa vituo  viwili vya kunyweshea mifugo.

Pia ameendelea kuwasisitizia wataalam waweze kuendelea kufanya usanifu wa mradi kwa kutumia Chanzo cha Mto Mwembamba ili kuendelea kuboresha huduma ya maji kwenye maeneo hayo pamoja na maeneo ya pembezoni

Naye Mbunge wa Jimbo la Longido Mheshimiwa Steven Kiruswa amepongeza Wizara ya Maji kwa kutekeleza kwa vitendo  kauli ya kumtua mama ndoo Kichwani.






Share To:

Post A Comment: