CHAMA cha ACT-WAZALENDO jimbo la Tanga pamoja na wakazi wa jiji la Tanga , leo agosti 11 wamejitokeza kwa wingi kuchangia Damu Salama kwaajili ya wagonjwa wanaopatiwa huduma kwenye Hospitali ya Rufani mkoa wa Tanga Bombo,
Uchangiaji huo wa Damu Salama umeenda sambamba na zoezi la uhamasishaji kwa jamii juu ya faida za uchangiaji wa Damu Salama ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani yanayofanyika kila Agosti 13 .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake chama hicho Mkoa wa Tanga Rehema Mohammed aliwaambia Waandidhi wa Habari kuwa Chama hicho kinatarajia Kufanya kongamano la Vijana agosti 13 ikiwa ni Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani hivyo katika kuelekea siku hiyo wameona nivyema kuokoa Maisha ya watu wengine,
‘’Kwakuzingatia umuhimu wa Damu hususani kwasisi wanawake chama chetu kimeona ni vyema kuokoa maisha ya watu wengine na tunaendelea kufanya hamasa hii kwa Wakazi wote wa Tanga kujitokeza kwa wingi kwenye uchangiaji wa Damu’’ Alisema Rehema
Sambamba na hayo Rehema alisema kabla ya maadhimisho hayo wanatarajiwa kufanya matukio mbalimbali ikiwamo kufanya mikutano ya Hadhara na makongamano yakuwaelimisha Vijana juu Mambo mbalimbali ya Nchi yao ikiwamo Uzalendo kwa Taifa.
Kwaupande wake katibu wa ngome ya Vijana ACT-WAZALENDO jimbo la Tanga Kassimu Hassan aliwashukuru Wananchi kwakuitikia wito wakuchangia Damu,
‘’Tunawashukuru wakazi wa Jiji la Tanga kwakujitokeza kwa wingi kuchangia Damu tunawaomba waeendelee kuwa Wazalendo kwakuhamasishana kuchangia zaidi ili tuokoe maisha ya wengine lakini hata sisi pia ni wagonjwa watarajiwa’’ Alisisitiza Kassimu
Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wanawake
chama hicho Mkoa wa Tanga
Rehema Mohammedakizungumza na wanahari kuhusu zoezi hilo la uchangiaji damu lililofanyika katika ofisi za chama hicho .
Wataalamu wa maabara kutoka katikahospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo wakitoa elimu ya uchangiaji damu wanachama wa ACT Waalendo waliojitokeza katika kushiriki katika zoezi hilo
Baadhi ya wanachama wa chama cha ACT Wazalendo waliojitokeza katika ofisi za chama hicho kuchangia damu salama leo augost 11,2023.
Post A Comment: