Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) akiwa anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Magharibi Zanzibar amesema Chama Cha Mapinduzi ndio Chama pekee kinachoweza kutatua kero za wananchi wake na kupitia Jumuiya zake ikiwemo Jumuiya ya Vijana. Ameyasema hayo tarehe 13 Agosti 2023 alipowasili Mkoa wa Magharibi Zanzibar.
"Sisi viongozi wenu hatupo katika nafasi kwa ajili ya kutafuta pesa bali tupo kwa ajili ya kuwatumikia nyinyi na kuonyesha uwezo wa Imani mliyotupatia kwa maana tulipokuja kuwaomba Kura tuliomba kura ili mtuchague na lengo la kutuchagua ni kwenda kuwasemea kero na shida zenu kwa maana kuna maeneo ambayo nyinyi hamuwezi kufika hivyo sisi tupo kwa ajili ya kuwasemea hizo changamoto zenu kwa maana tuna uwezo na nafasi ya kuweza kuzifikisha Changamoto na kero zenu moja kwa moja katika eneno husika na zikatatuliwa mara moja, wakati wengine hawawezi kuwa na uwezo na nafasi hiyo ya kutatua changamoto zenu".
Jumuiya ya Umoja wa Vijana inaendelea kujipambanua kwa kila kitu chini ya Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Rais Wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar hawa ni walezi wetu wapo na wana tuunga mkono Vijana wajibu wetu ni kuwa nasi kuwaunga Mkono kwa mambo makubwa wanayoyafanya ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Lakini pia nikiwa kama Kiongozi wenu wa Vijana ambaye mmenipa dhamana ya kuwaongoza ba kuwasemea lazima tuambiane baadhi ya mambo ambayo yatatupa nguvu ya kusonga mbele na kwa nguvu zaidi, nataka niwatie moyo Vijana wenzangu katika maisha hakuna kinachoshindikana kila kitu kinawezekana, na hata nyie mnaweza kuwa wenyeviti wa Vijana Taifa kwa maana hata mimi nilikuwa kama nyinyi, ila kikubwa msikate tamaa.
Mwisho nizidi kuwasisitiza Vijana wenzangu wa Dimani na wakitanzania wote, kikubwa kitakachotufikisha mbali ni sisi Vijana kuwa na nidhamu, uadilifu, na maadili ya hali ya juu ambayo ndio yanaelezea wewe ulivyo mtu wa aina gani na ndivyo utakavyofika mbali kwa kuzingatia haya.
Niwashukuru sana wana Dimani kwa mapokezi yenu mazuri katika Mkoa huu hakika niwaahidi mimi ni mtumishi wenu na nipo tayari kwa ajili ya kutumwa kwa maana ndio majukumu mliyonipa na ni lazima niyatimize kwa ufanisi wa hali ya juu zaidi.
Post A Comment: