Na Moreen Rojas,Dodoma.
Mkurugenzi wa Tume ya TEHAMA Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema hadi kufikia Juni 31 , 2023 TUME hiyo imesajili wataalam wa TEHAMA 1,600 wanaohudumia nchi nzima na bado zoezi la usajili linaendelea
Dkt.Mwasaga ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za TUME hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Akitaja Mafanikio kwa mwaka wa fedha 2023/24 amesema Tume imefanikiwa Kuanzishwa kwa mradi wa kujengwa kituo kikubwa cha Taifa cha Ubunifu Dar Es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma kwa wataalam, watafiti, na wabunifu wa TEHAMA.
"Tunatengeneza mfumo jumuishi utakaounganisha usajili na uendelezaji wa wataalam na wabunifu TEHAMA nchini (ICT human capital development system): lengo la mfumo huu ni kutambua bunifu na kupanua wigo wa ukuzaji wa wabunifu na bidhaa na huduma za TEHAMA zinazozalishwa Tanzania na hivyo kukuza pato la Taifa na kuongeza fursa za ajira kupitia TEHAMA na maendeleo ya kidijitali duniani"Amesema Dkt.Mwasaga
Aidha ameongeza kuwa wanaandaa mkutano wa mwaka wa TEHAMA (TAIC) na Tuzo ya TEHAMA Tanzania (Tanzania ICT Award)
"Hili lilikuwa kongamano kubwa la mwaka la TEHAMA lililofanyika Zanzibar mwezi Oktoba, 2022 na kuwashirikisha wawekezaji na wadau mbalimbali wa TEHAMA kutoka ndani na nje ya nchi wapatao 1,200"
Sanjari na hayo vipaumbele vya tume kwa mwaka 2023/24 ni pamoja na kuendelea na ukamilishwaji wa vituo vya ubunifu TEHAMA (Soft centers) katika Kanda 5 pamoja na kuanzisha kituo kimoja Zanzibar,kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT Refurbishment and Assembly centre),kuwezesha uanzishaji wa vituo vya majaribio vya ubunifu TEHAMA (District ICT Startups Innovation hubs) katika Wilaya 10,
Aidha vipaumbele vingine ni kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA nchini na kufanya tathmini ya kitaifa ya hatua za utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya TEHAMA,kuratibu na kuandaa matukio ya kuvutia uwekezaji na kutangaza masoko ya bidhaa za TEHAMA ndani na nje ya nchi,kushirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za TEHAMA ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini pamoja na kujenga kituo cha Artificial Intelligence kwa ajili ya kuendeleza wataalam wa TEHAMA.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Ndugu Gerson Msigwa amesema Serikali imeamua kuwekeza kwa nguvu kwenye Tanzania ya Kidigitali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo usimamizi m kuu unafanywa na Tume ya TEHAMA.
Ameongeza kuwa hili ni jambo kubwa kwani fedha nyingi imewekezwa kwa ajili ya kuboresha TEHAMA nchini kwani shughuli mbalimbali kwa sasa duniani zinafanyika kwa njia ya kidijitali ikiwemo huduma za malipo mabalimbali, huduma za afya za matibabu, uzalishaji, kilimo, uchimbaji wa madini.
Post A Comment: