Na; Moreen Rojas, Dodoma.


Katika kudhibiti na kuongeza usimamizi katika shughuli za uchimbaji wa madini nchini,tume ya madini imefanikiwa kutoa mafunzo kuhusu masuala ya usalama,afya,mazingira pamoja na usimamizi wa baruti kwa wachimbaji wadogo wa madini katika mikoa ya Singida,Dodoma,Mara na Kigoma.


Hayo yameelezwa na Mhandisi Ramadhani Lwamo Kaimu katibu mtendaji tume ya madini wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katika ukumbi wa idada ya habari maelezo kueleza mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya tume ya madini kwa kipindi cha mwaka 2022/23 na mikakati ya mwaka 2023/24.


Aidha tume ya madini katika kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na rasilimali madini imeendelea kusimamia uwasilishaji wa mipango ya ushirikishwaji wa watanzania katika sekta madini(LCPs)kutoka kwa wamiliki na waombaji wa leseni za madini pamoja na watoa huduma kama takwa mojawapo la sheria ya madini sura ya 123.


"Katika kipindi kinachorejewa jumla ya mipango 656 ya ushirikishwaji wa watanzania ilipokelewa na kufanyiwa uchambuzi,kati ya mipango iliyowasilishwa,652 ilikidhi vigezo na kuidhinishwa pia".Amesema Mhandisi Ramadhani


Aidha amesema kuwa wanaendelea kuelimisha Umma na kuboresha mawasiliano kati ya tume ya madini na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya madini,tume imefanikiwa kufanya utayarishaji wa vipindi maalumu na makala zinazohusu maudhui ya ndani na mchango wa kampuni za uchimbaji madini katika jamii kupitia programu za CSR katika mikoa 15 ambazo zilirushwa kwenye vituo vya redio na luninga pamoja na kuchapishwa katika tovuti na mitandao ya kijamii.


Aidha vipindi hivi vimeendelea kuelimisha Umma kuhusu masuala ya madini nchini ili kufungua fursa kw a watanzania kunufaika na rasilimali madini.


" Muelekeo wa sekta ya madini unalenga katika kuhakikisha mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa unafikia asilimia 10 au zaidi ifikapo mwaka 2025 kama inavyofafanuliwa katika dira ya maendeleo ya taifa,ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020 pamoja na mpango mkakati wa tume ya madini wa mwaka 2019/20 _2023/24 katika kuhakikisha azma hiyo imefikiwa"Amesisitiza Mhandisi Ramadhani.


Pamoja na mafanikio makubwa ya sekta ya madini bado kuna changamoto ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo wa sheria ya madini sura ya 123 na kanuni zake kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini na umma kwa ujumla hivyo kusababisha uwepo wa migogoro ya mara kwa mara.


Aidha katika mkakati wa utatuzi time imejipanga kuendelea kutoa elimu ya sheria za madini pamoja na kuendesha mafunzo ya mara kwa mara katika maeneo ya wachimbaji wadogo na viongozi wa serikali za mitaa ili kujenga uelewa wa sheria hiyo na kupunguza migogoro baina ya wachimbaji.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: