Msafara wa Wanafunzi, Walimu na viongozi wapatao 440 kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza safari kuelekea nchini Rwanda kushiriki Mashindano ya 21 ya michezo ya shule za Msingi na Sekondari wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA).
Safari hiyo imeanza leo Agosti 17, 2023 katika Shule ya Tabora girls mkoani Tabora kuelekea katika Mji wa Huye nchini Rwanda kupitia mpaka wa Rusumo.
Mashindano hayo yataanza tarehe 17-27 Agosti 2023 ambapo Tanzania itashiriki katika michezo ya Soka, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu, Hockey, Tennis, Riadha, Mpira wa Mikono na Netboli.
Nchi zitakazoshiriki ni pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rwanda, DR Congo, Kenya, Uganda.
Post A Comment: