Wadau mbalimbali wanaoshiriki Maonesho ya Madini na Uwekezaji mkoani Lindi wamevutiwa na bidhaa zilizozalishwa na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) katika banda la Wizara ya Madini.
Baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na TGC kutokana na madini mbalimbali zilizopo katika maonesho hayo ni pamoja na hereni, Pete pamoja na bangili za mawe.
Pia, wadau wakitoa maoni kuhusu zinazotolewa na kituo hicho wameshauri kuwepo na vituo vya mauzo na mafunzo ya uongezaji thamani madini katika maeneo mbalimbali nchini ili kuongeza uelewa wa uongezaji thamani madini.
Kwa upande wake, Afisa Biashara kutoka TGC Ofro Sanga ametoa fursa kwa wanafunzi kujaza fomu za kujiunga na mafunzo ya uongezaji thamani ngazi ya Stashahada katika Teknolojia ya Vito na Usonara yanayotarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2023 jijini Arusha.
Mafunzo mengine yanayotolewa ngazi ya cheti ni utambuzi wa Madini ya Vito, usonara, ukataji na ung'arishaji madini ya vito kwa mtu mwenye nia ya kujifunza.
Post A Comment: