Na
Mwandishi Wetu,Kibaha
KAMANDA wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) Mkoa wa Pwani Christopher
Myava amesema kuwa wamegundua kuwa baadhi ya wazabuni wamepewa
kazi na Afisa Manunuzi wa Halmashauri pasipo
kuomba kazi hizo kwa kupitia
mfumo wa manunuzi ya umma yaani
TANEPs.
' Hatua hii
imesababisha wazabuni kupata kazi
bila kufuata taratibu za
manunuzi ya umma mfano mzabuni
aliyechaguliwa kuleta vifaa vya ujenzi
katika shule mpya ya Sekondari ya Kata ya
Shungubweni iliyoko Wilaya ya Mkuranga
hakuomba kazi hiyo kwenye mfumo wa wa TANEPs na badala yake amepatiwa zabuni na Afisa Manunuzi
wa Halmashauri kinyume cha
utaratibu" amesema Kamanda wa
TAKUKURU Pwani Myava
"TAKUKURU
Mkoa wa Pwani tumegundua uwepo wa Kamati hewa
kwa baadhi ya miradi inayosimamiwa
na Halmashauri jambo limesababisha
uwepo wa mianya ya rushwa katika malipo yanayofanyika, jamii kutokuwa
na umiliki wa miradi hiyo kutokana na
kutokusbirikishwa katika
utekelezaji wake, mfano ujenzi wa Kituo
cha Afya Kisiju hamii
haikushirikishwa kabisa katika yaimamizi na utekelezaji wa mradi huu" amesema Kamanda Myava.
Aidha TAKUKURU
wamebaini mianya ya ukosefu wa
uaminifu katika kukusanya ushuru na
usimamizi uendeshaji wa soko la Mnarani Halmashauri ya Mji Kibaha imebainika kuwa wakusanyaji wa ushuru
kutotoa risiti za mashine ya POS baada
ya wafanyabiashara kufanya malipo
kwa kisingizio cha cha ubovu wa mashine
au mashine kutokuwa na 'Charge'
jambo ambalo limesababisha
wakusanyaji kutumia fedha hizo kwa matumizi yao binafsi na kusababisha kukosekana kumbukumbu za wafanyabiashara
waliofanya malipo yao" amesema Kamanda Myava.
"Upotevu
wa mapato ya maegesho unasababishwa
na utendaji mdogo wa
wakusanya mapato ambapo baadhi ya wakusanyaji hutoza viwango tofauti vya ushuru wa malori
yanayoegesha sokoni tofauti na
viwango vilivyowekwa kwenye sheria
ndogo" amesema Kamanda Myava.
Kamanda
Myava amesema tayari wamekaa kikao na wadau wa soko la Mnarani na kuweka maazimio moja wapo likiwa kukusanya
mashine zote ambazo zinadaiwa kuwa mbovu ili kudhibiti huo mwanya, wafanyabiashara wamepewa elimu ili.kuhakikisha wanadai risiti baada ya kufanya malipo ya ada na ushuru na
kutakiwa kutoa taarifa pindi
wanapoelezwa na wakusanya ushuru kuwa mashine zA POS ni mbovu ili kudhibiti upotevu wa mapato yanayokusanywa".
Pia wamekubaliana kutengeneza vibao vitakavyo
onesha bei za tozo za maegesho ili
kuepusha kutoza viwango tofauti hususani
kwa kila lori linapoegeshwa sokoni kwa
ajili ya kushusha bidhaa.
Kamanda
wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Myava amesema hayo leo Agosti 16 alipozungumza na Waandishi wa Habari kwenye Mkutano uliofanyika ofisini kwake
Kibaha " Kipindi cha robo
ya Aprili hadi Juni 2023,Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Pwani
tumeendelea na majukumu yetu
katika maeneo ya uzuiaji rushwa ,uchunguzi pamoja na
uelimishaji" amesema.
Amesema kuwa uchunguzi umefanyika wa tuhuma
mbalimbali huku tayari kesi imefunguliwa Mahakamani dhidi ya Afisa Manunuzi
wa Halmashauri ya Mkuranga .
Amesema kuwa katika eneo la uzuiaji rushwa wamefanya ufuatiliaji miradi 11 ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi.Bilioni mbili milioni mia tatu na
mbili na laki tano hamsini na mia
nne ishirini na sita
(2,302, 550,426/-) katika sekta za elimu, afya, maji barabara , masoko na amendeleo ya jamii, katika ufuatiliaji
wa utekelezaji wa miradi hiyo hakukuwa na mapungufu yaliyobainika katika miradi
hiyo iliyofanyiwa ufuatiliaji.
Ili kudhibiti mianya ya rushwa katika
Idara za serikali na sekta
binafsi tumefanya mikutano ya hadhara 36, semina nane
kwa watumishi wa serikali
na sekta binafsi imefanyika,maonesho nane yamefanyika,.klabu za
wapinga rushwa 96 zimeimarishwa kwenye shule
za msingi na sekondari na elimu dhidi ya rushwq imetolewa
kupitia vipindi bitatu vya redio.
Amesema
kuwa idadi ya malalamiko yaliyopokelewa ni 87,malalamiko yanayohusu rushwa 62, yasiyohusu rushwa 25, malalamiko yaliyohamishiwa Idara
nyingine 04, yaliyoshauriwa 18 na
yaliyofungwa hakuna.
TAKUKURU Mkoa wa Pwani imeweka mikakati yake
katika kipindi cha Julai hadi Septemba
2023 kuwa ni kiendeleza programu ya TAKUKURU Rafiki, kuendelea kufanya
ufuatiliaji na chambuzi za mifumo
kwa lengo la kuziba mianya
ya rushwa itakayobainika
kuendelea kukagua utekelezaji
wa miradi yote ya maendeleo ndani
ya Mkoa wa Pwani.
Kuendelea kuelimisha umma wa watanzania juu ya madhara ya rushwa ili wafahamu nafasi yao katika mapambano
dhidi ya rushwa kwa makundi yote katika jamii kuendelea nauchunguzi
wa vitendo vya rushwa na
kuchukua hatua za kisheria
dhidi ya wale watakaobainika kutenda makosa ya rushwa.
Kamanda wa TAKUKURU Pwani Myava ametoa wito na kuwahamasisha wananchi na wadau wote katika Taasisi za serikali na sekta binafsi kuendelea
kuunga mkono juhudi za
mapambano dhidi ya rushwa kwa kukataa kujihusisha na vitendo
vya rushwa ,kufuatilia miradi ya
maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili thamani ya fedha ya serikali ionekane
na kwakufanya hivyo miradi ya
maendeleo itatekelezwa kwa kiwango kilichokusudiwa na hivyo kuleta maendeleo
na huduma bora kwa wananchi, pia
wananchi wanaombwa kutoa taarifa za
vitendo vya rushwa endapo utavishuhudia au kusikia
ili wahusika wachukuliwe hatua za
kisheria 'Kuzuia rushwa ni jukumu lako
na langu, tutimize wajibu wetu'
Post A Comment: