SMAUJATA mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na kampuni ya AGRICULTURE BUSINESS COMPANY (ABC) wameweka mpango mkakati wa kuanzisha mradi wezeshi wa kilimo, mafunzo ya uzalishaji bidhaa mbalimbali, ufugaji wenye tija sambamba na kupewa ruzuku ya mikopo isiyo umiza huku moja ya wanufaika wa mradi huo wakitajwa kuwa ni vijana na akinamama wanaolea watoto pasipo wazazi wenzao (Single Mother).
Akizungumza mara baada ya kukutana na uongozi wa SMAUJATA mkoani humo Makamu mkuu Idara ya mipango SMAUJATA ngazi ya taifa Hekima Msigwa ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji mkuu wa kampuni hiyo ya ABC amesema wakati umefika wa kampuni ya ABC na SMAUJATA kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwainua wanawake hao na vijana ambao katika kipindi cha mradi watakuwa chini ya uangalizi wa ABC na SMAUJATA mpaka pale watakapo weza kujitegemea wao wenyewe.
Sanjali na hilo pia Bw. Msigwa amesema ili viongozi wa SMAUJATA waweze kufanya kazi kwa urahisi atahakikisha wanapata ofisi zao binafsi kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha viongozi hao kufanya kazi kwa urahisi na kuifikia jamii kwa urahisi pia huku akitoa pongezi kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum Dorothy Gwajima kwa kuanzisha kampeni hii, Mwenyekiti SMAUJATA Taifa Sospeter Bulugu na Mwenyekiti mkoa wa Njombe Damian Kunambi.
Hata hivyo Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Njombe Damian Kunambi awali akiwasiliana na Mkurugenzi huyo alimpongeza kwa ushirikiano wake na mashujaa wa SMAUJATA na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kampuni hiyo ili kuweza kuisaidia jamii kukua kiuchumi na kuondokana na migogoro ya uchumi duni ambayo imekuwa ni moja ya chanzo cha vitendo vya ukatili.
Aidha miongoni mwa viongozi walioshiriki katika kikao hicho ni Makamo Mwenyeki wa SMAUJATA mkoani humo, Witness Kihenzile, Katibu SMAUJATA mkoa Robert Matimbwa pamoja na Lilian Mhelela ambaye ni katibu Idara ya elimu mkoani Njombe.
Post A Comment: