Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi, Rashid M. Rashid (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Singida walipomtembelea ofisi kwake Agosti 29, 2023 kwa ajili ya kuzungumzia kongamano hilo litakalofanyika Oktoba 7, 2023.
.................................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHUJAA wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Singida wanatarajia kufanya kongamano
kubwa la wazi na la kihistoria ambalo pamoja na mambo mengine litajadili suala
la uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam, ukatili wa kijinsia na mambo mengine
ambapo linawaomba wadau mbalimbali kusaidia kuchangia Sh. Milioni 11.5 kwa
ajili ya kufanikisha kongamano hilo.
Kamati ya maandalizi ya kongamano hilo wakiongonzwa na Mwenyeki wa Smaujata
Mkoa wa Singida, Dismas Kombe wameeleza nia ya kongamano hilo walipokutana na
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi, Rashid M. Rashid , Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo, Haika Masawe, Afisa Ustawi wa Jamii wa wilaya hiyo,
Robby Muhochi pamoja na Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo Mrakibu wa Polisi (OCD),
Suzana Kidiku.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Amrani akizungumza lengo la kongamano hilo
ambalo litafanyika Oktoba 7, 2023 Stendi ya Mabasi ya zamani mjini hapa na kuwa na watu
zaidi ya 1000, alisema ni kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia,
uchangiaji wa damu salama, elimu kuhusu mkataba wa Bandari ya Dar es Salaam,
dira ya maendeleo ya Taifa letu kuanzia mwaka 2025/ 2050.
Amrani alitaja mambo mengine yatakayokuwepo kwenye kongamano hilo kuwa ni
elimu salama mashuleni hasa kwa mtoto wa kike na kupunguza alama ziro na kwamba
watakuwepo wataalamu mbalimbali wakiwemo Maafisa Ustawi wa Jamii na maendeleo
ambao watatoa mada.
Alisema kuwa katika kongamano hilo kutakuwa na viongozi wa Serikali, dini
wananchi, wanafunzi na kuwa litanogeshwa na burudani za aina tofauti tofauti
kama muziki wa kizazi kipya, asili, mashairi, ngonjera na nyimbo ambazo
Smaujata wataziandaa zenye mafundisho ya kupinga ukatili.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Omari Mwangi alisema wanaamini kupitia
kongamano hilo jamii itapata elimu na kupunguza kama sio kumaliza vitendo vya
ukatili vilivyokithiri kutokana na kumomonyoka kwa maadili ambapo kwa upande
mwingine kunachangiwa na wazazi au walezi.
'' Wazazi wengi wamekuwa wakikwepa majukumu ya malezi ya watoto wao na
kuwaacha wafanye mambo yao jambo ambalo limewafanya wajikute wakiingia katika
makundi yasiofaa na kuanza kufanya vitendo vilivyo kinyume na maadili,''
alisema Mwangi.
Makamu Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Singida, Ambwene Kajula alisema kuwa
lengo la kongamano hilo ni kuwapata viongozi ili wapate majibu ya moja moja
kutoka na changamoto mbalimbali walizonazo wananchi dhidi ya vitendo vya
ukatili wa kijinsia.
'' Tuliona kongamano itakuwa njia rahisi ya kuwakutanisha wananchi wengi na
viongozi wao wengi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Singida ili wajue changamoto
zao pia itakuwa ni fursa kwa Smaujata kujitangaza,''.
Alisema pamoja na jitihada kubwa inayofanywa na Smaujata ya kupambana na
vitendo vya ukatili bado elimu haijawafikia watu wengi na kupitia kongamano
hilo wataweza kuipata kupitia michezo ya kuigiza na kuwa kutakuwa na makala
maalumu ya video 'Ducumentary' ambayo itaonesha watu wakitoa shuhuda za ukatili
wa kijinsia na hatua zilizochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa vitendo hivyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo Mrakibu wa Polisi (OCD),
Suzana Kidiku aliwapongeza Smaujata kwa kuandaa kongamano hilo ambalo linakwenda
kuwa msaada katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na uharifu.
Alisema katika wilaya hiyo kumekuwa na wimbi kubwa la watoto ambao
wanafanya uharifu mkubwa jambo ambalo linaleta changamoto kubwa ya kuwahifadhi
kwani hawawezi kuwaweka mahabusu ya watu wakubwa kulingana na sheria
zinazowalinda.
Mkuu huyo wa wilayani humo alisema kukithiri kwa utoro wa watoto mashuleni ndio chanzo kikubwa cha
kujiingiza kwenye vitendo vya uharifu huku matukio ya ubakaji na ulawiti
yakiongeza kila kukicha.
Aidha, Kidiku alisema ili kuthibiti utoro huo wameanzisha utaratibu kwa watoto
vinara wa utoro kusaini kila asabuhi wanapofika fika shuleni na wanapotoka
katika daftari maalum litakalokuwa kwa mkuu wa polisi wa kata ilipo shule
husika wanazosoma ambapo pia litakuwa likisainiwa na mwalimu wa darasa la
mwanafunzi na kuwa utaratibu huo wamehusishwa na wazazi wao.
Katika kuwaunga mkono Smaujata, Kidiku aliahidi kutoa kiasi cha fedha ambazo zitasaidia kununulia maji
ya kunywa wakati wa kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Singida, Dismas Kombe aliwashukuru viongozi
wa wilaya hiyo kwa mapokezi mazuri waliowapa na akawaomba wadau wengine
kujitokeza kusaidia ili wapate kiasi hicho cha fedha.
Alisema kwa mtu yeyote, Taasisi, Wafanyabiashara, makundi mengine na
madhehebu ya dini watakao kuwa tayari wana weza kuwasiliana na waratibu ,
Dismas Kombe kwa namba ya simu 0758489886, Mwenyekiti wa Kongamano, Juma Amrani
kwa namba 0763850879 na Makamu Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Singida, Ambwene
Kajula kwa simu namba 0713343687 na Makamu
Mwenyekiti wa kongamano hilo, Omary Mwangi kwa namba ya simu 0782651919.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Amrani alimpongeza Mwenyekiti wa Smaujata
Wilaya ya Ikungi, Hussein Mseule kwa kuratibu ziara hiyo ambayo imeonesha
mafanikio makubwa na mapokezi mazuri ya kamati hiyo.
Kamati hiyo inatarajia kuendelea na ziara hiyo ya kuwaomba wadau kuchangia
kongamano hilo katika Wilaya za Mkalama, Iramba, Manyoni na Itigi.
Timu nzima ya Smaujata ambayo ilishiriki kwenye ziara hiyo ni Wajumbe wa
kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Omari Mwangi Makamu Mwenyekiti,
Mwenyekiti Juma Amrani, Katibu, Beatrice Claud na Mweka Hazina Elineema Babu.
Wengine ni Katibu wa Smaujata Mkoa wa Singida, Patrick Msinda, Katibu wa Smaujata Wilaya ya Ikungi, Maxwell Ngwallo, Ester Issaya na Rehema Mangula.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi, Rashid M. Rashid.]wa sita kutoka kushoto}
Post A Comment: