Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mamla ya Majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) imetoa mapendekezo ya marekebisho ya Bei za Maji kwa muda wa Miaka mitatu  ikiwa lengo ni kutatua changamoto zilizopo na kukidhi gharama za uzalishaji na usambazaji wa Maji.

Akiwasilisha mapendekezo hayo Mkurugenzi wa SHUWASA Mhendisi Yusuph Katopola amesema marekebisho hayo yatasaidia kujiendesha kwa faida na kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.

Amefafanua kuwa bei hizo zitaiwezesha mamlaka hiyo kuwa na uwezo mzuri wa kifedha ili kukidhi gharama za uzalishaji na usambazaji wa Maji pamoja na gharama ya ununuzi wa Maji kutoka KASHWASA.

Amesema SHUWASA imelenga kuongeza mtandao wa maji na kuyafikia maeneo yote yenye uhitaji wa huduma hiyo ambapo pia amebainisha bei zilizopendekezwa kwa makundi mbalimbali.

“Bei tulizopendekeza kwa kundi la wateja wa majumbani ni shilingi 2550/= Mwaka (2023/2023), sh 3,190/= Mwaka (2024/2025) na 3,630/= Mwaka (2025/2026) kutoka sh. 1740/= kwa sasa  unit moja na huduma za kurejeshewa huduma ya maji baada ya kusitishiwa kutoka sh. 10,000/= hadi sh. 15,000/= lakini ada za maunganisho mapya ya huduma ya maji hii hatujapendekeza makundi yote yataendelea kutoa asilimia 20 ya vifaa vya maunganisho”.amesema Mkurugenzi SHUWASA Mhandisi Katobola

Mhandisi Katopola amezitaja sababu za kuomba marekebisho ya bei za maji kuwa ni pamoja na kuisha kwa muda wa bei za awali, kuongezeka kwa bei ya jumla ya kununua maji kutoka KASHWASA, uwepo wa kodi na ushuru mbalimbali, kupanda kwa gharama za uendeshaji kuongezeka kwa maeneo ya kutoa huduma.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa  SHUWASA imelenga kusafirisha maji safi na bora kwa wateja, kuendelea kusambaza mabomba hadi kwenye maeneo ya nje ya mji, kujenga mitambo ya kuchakata majitaka ambapo amesema changamoto zilizopo ni pamoja na mwamko mdogo wa wananchi kulipia bili ndani ya siku 30.

Wananchi walioshiriki mkutano huo wamekuwa na maoni tofauti kuhusu mapendekezo hayo ambapo baadhi yao wameonesha kuridhishwa na mapendekezo hayo huku baadhi wakionesha kutoridhishwa.

Mwakilishi kutoka Baraza la ushauri la serikali (GCC) Mr. Julius Mwambaso ametoa ushauri unaolenga kumsaidia mtumiaji wa maji huku akiisisitiza mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga SHUWASA kutekeleza kwa vitendo yale watakayokubaliana.

“Sisi wataalam au Baraza ambalo linawataalam wote rimeridhishwa na ukokotoaji msisitizo tu tunaweka ni kwamba ni kuhakikisha SHUWASA mnatekeleza kwa vitendo haya mambo yote ambayo mmeyasema kuwa mtayafanya”.amesema Mwambaso

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na Maji EWURA CCC Bwana Joseph Ndatala ametoa ushauri wake.

“Kwa kuwa bei za maji za SHUWASA kwa sasa ziko juu zitaumiza wateja hawa ambao wengi wao ni wenye kipato cha chini hivyo Baraza la EWURA CCC linashauri bei hizo zibaki hivyo hivyo  kama zilivyo kwa sasa lakini pia Baraza linashauri pawepo na ongezeko dogo tu ambalo halitakuwa na madhara kwa watumiaji katika makundi haya”.amesema Ndatala

Awali mgani rasmi wakati akifungua mkutano huo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude amesema hatua hiyo itachochea ufanisi katika utoaji wa huduma kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA).

DC Mkude ametumia nafasi hiyo kuwaomba watumiaji wa maji kutoa maoni yao kwa kujenga hoja bila upendeleo na kuhakikisha wanashirikiana ili kuwa na makubaliano ya pamoja.

Meneja wa EWURA kanda ya ziwa  George Mhina amesema mkutano huu ni sehemu ya uchunguzi unaofanywa na EWURA kwa lengo la kupata maoni ya wadau wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kabla ya kutoa maamuzi kuhusu maombi yaliyowasilishwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga SHUWASA ambapo amesema  utaratibu huo wa kukusanya maoni ni moja ya njia za kutekeleza azma ya Serikali ya utawala bora kwa maana ya kuwashirikisha wananchi katika kufanya maamuzi.

Mamlaka ya uthibiti wa huduma za nishati na maji imefanya mkutano na wadau wake kwa lengo la kupokea maoni kuhusu maombi ya marekebisho ya bei yaliyowasilishwa na SHUWASA ambapo zoezi la kupokea maoni litaendelea kwa njia ya maandishi hadi Agosti 29 Mwaka huu 2023.

 

Mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhendisi Yusuph Katopola akiwasilisha mapendekezo ya bei za maji kwa wadau leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Meneja wa EWURA kanda ya ziwa  George Mhina akizungumza kwenye taftishi iliyolenga kupokea ombi la kurekebisha bei za maji kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkunde awali akifungua mkutano huo uliolenga kupokea mapendekezo ya bei mpya za maji leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mwakilishi kutoka Baraza la ushauri la serikali (GCC) Mr. Julius Mwambaso akitoa ushauri kwenye mkutano huo leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mwakilishi kutoka Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na Maji EWURA CCC Bwana Joseph Ndatala akitoa ushauri kwenye mkutano huo leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

 

Mkutano ukiendelea leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga 






Zoezi la wananchi na wadau mbalimbali kuwasilisha maoni yao juu ya bei za maji likiendelea katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhendisi Yusuph Katopola akijibu maswali yaliyoulizwa kwenye kikao hicho  leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.



Share To:

Misalaba

Post A Comment: