Na; Moreen Rojas, Dodoma.                         


Kupitia mfuko wa elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA katika mwaka wa fedha 2022/2023 shilingi 10.99 ziligharimia ufadhili wa miradi wa miradi 132 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule 151 nchini.                       



Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya elimu Tanzania (TEA)Bi.Bahati Geuzye katika mkutano wa wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukimu ya mamlaka hiyo katika ukumbi wa mikutano wa idara ya habari maelezo jijini Dodoma.                                                 


Aidha amesema kuwa miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa madarasa 114 katika shule 38 za msingi na sekondari 02 maabara 10 za sayansi katika shule 05 za sekondari 08 miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na utoaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika shule 08 za msingi.     


 

 "Miundombinu hiyo imehusisha ujenzi wa madarasa ujenzi wa madarasa 10 matundu ya vyoo 50 na mabweni 03 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum,miradi mingine iliyotekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/23 ni pamoja na ujenzi wa nyumba 52 za walimu katika shule 13 za msingi 7 na sekondari 6 pamoja na ujenzi wa majengo ya utawala 7 katika shule sita za sekondari na moja ya msingi,miradi hiyo imenufaisha jumla ya wanafunzi 22,556 na walimu 123 nchini kote".     



Aidha amesema kuwa TEA ambayo ni miongoni mwa Taasisi za Muungano kupitia mfuko wa elimu imetoa ufadhili wa sh.Milioni 500 kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa miundombinu pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika vyuo viwili vya Elimu ya juu vilivyopo Tanzania Zanzibar.                                          


" Katika ufadhili huo,taasisi ya karume ya sayansi na Teknolojia (KIST) ilipokea ufadhili wa shilingi Milioni 200 na chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kampasi ya Benjamin Mkapa iliyopo Pemba kilipokea ufadhili wa Sh.Milioni 300 ufadhili huo umenufaisha wanafunzi 700 katika vyuo hivyo viwili".                           




Katika kuunga mkono azma ya serikali ya kuhamishia makao makuu ya nchi jijini Dodoma TEA kupitia mfuko wa elimu ilifadhili miradi mikubwa miwili ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Msingi inayofundisha kwa lugha ya kiingereza ya Msangalee kwa thamani ya Sh.Milioni 750 katika mwaka 2021/22 mradi huo umekamilika katika mwaka wa fedha 2022/23,mfuko ulifadhili ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu katika shule nne za msingi jijini Dodoma ambazo ni Kisasa,Kizota,Medali na Mlimwa C kwa thamani ya Sh.Bilioni 1.9 mradi huu ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha.                        



Aidha katika mwaka wa fedha wa 2022/23 TEA ilipokea michango na kutekeleza miradi ya pamoja na mashirika ya Umma na yasiyo ya kiserikali yenye thamani ya Sh.Milioni 404,mashirika hayo yaliyoshirikiana na TEA ni pamoja na shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA),BRAC Maendeleo Tanzania,Taasisi ya Asilia Giving,Taasisi ya Flaviana Matata,Taasisi ya SAMAKIBA,CAMARA Education Tanzania na Kampuni za Sayari Safi na Dash Industries Ltd.                             



Utekelezaji wa miradi chini ya mfuko wa kuendeleza Ujuzi (SDF) katika awamu ya kwanza ya ESPJ umekamilika ambapo serikali imefanikiwa kufikia malengo yake ya utekelezaji kwa kiwango cha juu,ikiwa ni pamoja na kufikia jumla ya wanufaika 49,063 sawa na 114% ya wanufaika waliolegwa,programu za mafunzo ya ujuzi zilizofadhiliwa na mfuko wa kuendeleza ujuzi zimeweza kunufaisha wanawake 22,413 sawa 46% na wanaume 26,650 sawa na 54% ya wanufaika wote.                  




Aidha vijana walionufaika ni pamoja na vijana 464 waliotoka kundi la wenye ulemavu,vijana 2,928 walitika kundi la vijana kutoka kaya maskini na wanaoishi katika mazingira magumu kwa upande wa Tanzania bara na 600 waliotoka kundi la vijana kutoka kaya maskini na wanaoishi katika mazingira magumu walinufaika kwa upande wa Tanzania Zanzibar,Ufuatiliaji wa wanufaika wa programu za mafunzo ya ujuzi yaliyofadhiliwa na SDF umeonyesha kuwa 80% ya wanufaika wameweza kujiajiri au kuajiriwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.



Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: