Na ; Elizabeth Paulo, Dodoma 

SERIKALI Yaja na Mradi wa Kukabiliana na Uharibifu wa Misitu ya Miombo ya nyanda kame.

Wataalamu wa Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Miombo ya nyanda kame (Integrated Landscape Management in the Dry Miombo Woodlands of Tanzania) wameketi kikao cha awali kujadili Namna watakavyokabiliana na Uharibifu wa Misitu Hiyo , Kikao kazi hicho kimefanyika Leo Agost 25,2023 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Morena Jijini Dodoma .

Akitoa Hutuba ya Kamishna wa Uhifadhi TFS Bw. Rogasian Lukoa Amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) wameanza kutekeleza mradi wa ufadhili wa Mfuko wa Mazingira ya Dunia – Global Environmental Facility- GEF 7.

Bw.Lukoa amesema kuwa Lengo kuu la mradi ni kukomesha na kubadili mwelekeo mbaya wa uharibifu wa ardhi na upotevu wa bioanuwai katika maeneo yaliyoharibiwa ya ukanda wa Misitu ya Miombo Kusini-magharibi mwa Tanzania.

"Mradi huu unatokana na Programme inayotekelezwa katika nchi 11 Angola, Botswana, Malawi, Mozambique, Namibia, Zimbabwe, Tanzania, Kenya, Burkina Faso, Mongolia na Kazakhstan. Kila nchi itapimwa kwa matarajio waliyojiwekea ambapoTanzania tutapimwa kwa uhifadhi mzuri wa Misitu ya Miombo na hatimaye kuleta tija kwenye mnyororo mzima wa Mazao ya nyuki na Maisha ya Jamii". Amesema Bw.Lukoa






Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: