Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Serikali imeridhia Kuboresha sekta ya Kilimo nchini ikiwa ni Pamoja na Kuboresha huduma za ugani ambapo kanda ya kati imenufaika na Pikipiki, Mizani ya kupima uzito wa mazao na mifugo, Teknolijia za umwagiliaji na magari ya Usimamizi wa shughuli za Umwagiliaji, Vifaa kinga kwa Manufaa ya Ugani na Ruzuku za mbegu bora za mazao.

Aidha Viuatilifu vya kudhibiti wadudu waharibifu na mazao ya mifugo, Ujenzi wa Mabwawa ya Umwagiliaji, Malango na Mabirika ya kunyweshea mifugo, Maboresho kwenye sekta ya Uvuvi Pamoja na Maboresho ya majosho na Minara ili kuongeza tija ya ufugaji na uzalishaji.

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Pateobas Katambi amesema hayo leo Agost 8,2023 Jijini Dodoma wakati akifunga Sherehe na maonesho ya Kilimo, Mifugo, Na Uvuvi nanenane Kanda ya kati katika viwanja vya Nzuguni Kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Katambi amesema mchango wa ukuaji wa kiuchumi utokanao na shughuli za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu umepungua sana kutoka 3.9% mwaka 2021 hadi 3% mwaka 2022.

Amesema Mchango wa shughuli za Kilimo katika pato la Taifa umepungua kutoka 26.8% mwaka 2021 hadi 26.2% mwaka 2022. 

“Mchango wa Sekta hizi umepungua kutokana na ugonjwa ulioikubwa Dunia mzima (UVICO 19) Pamoja na Mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyojitokeza na kuathiri shughuli za uzalishaji. ” Amesema Katambi

Katika hatua nyingine Naibu Waziri amesema maonesho ya nanenane yanatoa mwanya wa kuleta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayokabili uzalishaji na biashara mnyororo wa thamani wa sekta hizo.

“Ndiyo maana serikali imeweka utaratibu wa maonesho haya kufanyika kila mwaka na kutengewa muda wa wiki nzima ili kutambua kwanza mchango mkubwa wa Wakulima, Wafugaji na wadau wote katika sekta hizi .”Ameeleza Katambi

Hata hivyo amesema Sekta hiyo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa katika kupunguza umaskini na kuhakikisha usalama na uhakika wa upatikanaji wa chakula kwani zaidi ya asilimia 80% za watanzania wanategemea Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na ustawi wa maisha.

“lakini pia tunapata fedha za kigeni katika sekta ya Kilimo kwa bidhaa mbalimbali na huduma hata malighafi zinazo safirishwa zitokanazo na sekta ya Kilimo na ni fursa ya kipeke katika kufikia azma ya Tanzania kuwa kitovu cha chakula Afrika nakuwa na uchumi wa Viwanda”Amesema Katambi

Imebainishwa pia kuwa uwekezaji katika sekta hizo unamatokeo mapana ya kiuchumi na kijamii Mara nne ya uwekezaji wa katika sekta nyingine na hii ni kwasababu washiriki ni zaidi ya 80% katika mnyororo wa thamani utokanao na sekta hiyo.


Kadhalika ametoa Rai kwa Taasisi za kifedha kuangalia namna bora ya kukopesha Wakulima wadogo kwenye vikundi na wakulima binafsi kwa masharti rahisi kama kutumia miataba ya ununuzi wa mashamba mashamba na Viwanja Na mikataba ya masoko kama dhana za mikopo mbadala badala ya kuomba hati kubwa za nyumban au mali nyingine zenye thamani kubwa  kwani wakulima wengi Bado wanakosa hati hizo.



Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: